BAADHI ya wachezaji wa Yanga wanaocheza nafasi ya beki wa kati namba nne na tano wameanza kuingiwa na mchecheto wa kupata namba katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo kutokana na uongozi kuendelea kusajili wachezaji wanaocheza nafasi hizo.
Hali hiyo imekuja hivi karibuni baada ya klabu hiyo kuwanasa mabeki wawili, Kelvin Yondani kutoka Simba na Ladislaus Mbogo wa Toto Africa.
Usajili wa wachezaji hao unaifanya Yanga kufikisha wachezaji nane ambao ni Chacha Marwa, Nadir Haroub 'Cannavaro', Athumani Idd 'Chuji',Ibrahim Job, Zubery Ubwa, Bakari Mbegu, Yondani pamoja na Mbogo.
Wakizungumza na gazeti la Mwananchi kwa nyakati tofauti hivi karibuni, baadhi ya wachezaji hao (majina tunayo MwananchiCoLtd) walionekana kuwa na hofu ya kupata namba katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo.Hata hivyo msimu uliopita waliokuwa wanaanza katika kikosi cha kwanza walikuwa Nadir Haroub na Athumani Iddi
Walisema kwa sasa wanachosubiri ni timu kuingia kambini kujiandaa na michuano ya Kagame na huko ndipo watakapopata majibu sahihi ya maswali yao.
"Siwezi kuzunguza lolote kwa sasa juu ya hali hiyo kwa sababu mimi siyo kocha lakini majibu yatajulikana baada ya kuingia kambini hivi karibuni."
Kikosi hicho cha Yanga kinatarajia kuingia kambini leo kujiandaa na harakati zake za kutetea ubingwa wa mashindano ya Kagame ikiwa ni pamoja na mikikimikiki ya msimu ujao wa Ligi Kuu.
Yanga wakiwa mazoezini leo tarehe 18/06/2012 chini ya Kocha Msaidizi Fred F Minziro |
No comments:
Post a Comment