Facebook LIKE

Thursday, August 30, 2012

Mbuyu Twite atua rasmi Jangwani



Mbuyu Twite (mwenye jezi ya njano) 
Twite, Twite, Twite!!!!
Hayo ni maneno ya washabiki wa Yanga walikua wakiimba kumshangilia Twite mara baada ya kutua Uwanja wa Ndege wa mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.
Hakika ilikuwa ni furaha, vifijo na nderemo kwa watu waliofurika kumpokea mchezaji wao mpya Mbuyu Twite. 
Mbuyu Twite akiwa na katibu mkuu wa Yanga, Mwesigwa Selestine
Mchezaji mpya wa kimataifa wa timu ya taifa ta Rwanda ,Mbuyu Twite amewasili leo jijini Dar kutokea nchini Rwanda tayari kujiunga na mabingwa wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati timu ya Young Africans.
Twite aliwsali majira ya saa 10:15 kwa majira ya Afrika Mashariki kwa shirika la ndege la Rwanda Air na kupokelewa na viongozi wa Young Africans na washabiki wengi waliojitokeza kumpokea Uwanja wa ndege wa Mwl JK Nyerere.
Mara baada ya kuwasili mlango wa kutokea watu mashuhuri, Twite alipewa jezi ya Yanga yenye namba 4 mgongoni iiiliyoandikwa jina la Aden Rage, mwenyekiti wa Simba. 
Umati mkubwa ulijitokeza kiasi kilichopelekea Twite kushindwa kutokea mlango wa kawaida wa kupelekea uongozi wa uwanja huo kumuongoza Twite kutokea mlango wa wageni mashuhuri.
Msafara ulianza Uwanja wa ndege wa Mwl JK Nyerere kuelekea makao makuu ya klabu, huku magari yakiwa mengi, pikipiki na wengine wakitembea kwa miguu mpaka makao makuu ya klabu. 
Msafara uliendelea mpaka makao makuu ya klabu, kwa kupitia mtaa wa msimbazi ambapo wapenzi na washabiki wa simba hawakuweza kuamini macho yao mara baada ya kumuona Twite akiwa katika gari ndogo ya Yanga, na washabiki na wanachama wakiwazomea simba na kuwakejeli kwa maneno ya dhihaka.


Umati uliojitokeza kumpokea Mbuyu Twite, Uwanja wa Mwalimu JK Nyerere
Mara baada ya kufika makao makuu ya klabu ya Yanga, mchezaji Mbuyu Twite alipanda juu ghrorofani kuwasalimia washabiki na wanachama waliojitokeza kumpokea, kisha alikabidhiwa funguo ya chumba ambacho atakua akikitumia kwa kipindi chote atakachokuwa Yanga.
Mbuyu Twite amesema anajisikia vizuri, na furaha na mwenye bahati kuja kuchezea timu ya Yanga na anawaahidi kuonyesha kiwango cha juu kipindi chake chote atakaoitumikia Young Africans, Twite kesho anatajumuika na wenzake katika mazoezi asubuhi Uwanja wa Loyola kabla ya jumamosi kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Coastal Union.

Wednesday, August 29, 2012

Magoli ya mechi ya RealMadrid dhidi ya Barcelona haya hapa kama ulikosa mechi RealMadrid 2-1 Barcelona

Hili ni Goli la kwanza lililofungwa na Gonzalo Higuain wa RealMadrid

Gonzalo HiguaĆ­n goal(Real Madrid vs Barca 2nd leg supercup)Twitter @TheKSTYLES from Kelly Kelvin
on Vimeo.
Hili ndilo goli alilofunga Cristiano Ronaldo ambalo limeiwezesha RealMadrid kubeba kombe la kwanza msimu huu ni kombe la SuperCup linalokutanisha bingwa wa LIGI(RealMadrid) na bingwa wa KOMBE LA MFALME(Barcelona).Mechi ya kwanza Barca walishinda 3-2 nyumbani kwao ila ugenini wamefungwa 2-1 kwahiyo RealMadrid wamebeba kombe hilo kwa faida ya mabao ya ugenini

Real Madrid Vs Barcelona 2-1 Cristiano Ronaldo Fantastic Goal Spanish Super Cup 29-082012 (2nd leg)Twitter @TheKSTYLES from Kelly Kelvin on Vimeo.
HIGHLIGHTS ZA MABAO YOTE HII HAPA

2-1 Real Madrid highlights win its ninth Supercup Twitter @TheKSTYLES from Kelly Kelvin on Vimeo.

Wednesday, August 22, 2012

Video ya Marley ft. Belle9-Sina cha Kupoteza.Bonge la track hebu cheki


Marley ft. Belle9-Sina cha kupoteza from Kelly Kelvin on Vimeo.

Baadhi ya picha za duka la linalomilikiwa na rapper Soulja Boy alilolifungua hivi karibuni..!!

RAPPER TWISTA ALIJITOKEZA KUMSAPOTI SOULJA BOY 
BUN_B NAE ALIJITOKEZA KUMPA SAPOTI SOULJA BOY
SOULJA BOY AKIWA KATIKA DUKA LAKE
SOULJA BOY AKIWA NA MMOJA YA MASHABIKI WAKE KWENYE DUKANI LAKE
Add caption
BAADHI YA WATU WALIOJITOKEZA KWENYE DUKA HILO
SOULJA BOY AKIWA NA MASHABIKI WAKE
TUNECHI(LilWayne) nae
soulja boy


Na hichi ndicho alichokiandika kwenye Twitter account yake SOULJA BOY

Na kama upo Twitter waweza Kutufollow pia kupitia hapa;

Mshindi wa shindano la Bibi Bomba huyu hapaa....!!



 Shindano ambalo lilikuwa likionyeshwa na kuandaliwa na Clouds Media Group kupitia kituo chake cha CLOUDS TV.Ambapo baadhi ya mabibi walikusanywa na kuwekwa pamoja huku kila mmoja akionyesha kipaji,ufundi na utundu alionao na bibi aliyeibuka kidedea ndo kama unavyomuona hapo chini;
Veronica Mpangala  a.k.a Tukinao

Monday, August 20, 2012

Kigamboni ya miaka ijayo....!! Itakuwa kama hivi....!!Hebu cheki kama haukuiona hii


THE KIGAMBONI NEW CITY PLAN(Official) from Kelly Kelvin on Vimeo.

Yanga yaichakaza African Lyon katika Uwanja wa Taifa....!!


KIKOSI CHA YANGA DHIDI YA AFRICAN LYON
Mabao yaliyowekwa wavuni na Haruna Niyonzima,Simon Msuva,Jerry Tegete na moja la kujifunga yalitosha kuipa ushindi wa mabao 4-0,Mabingwa wa Kombe la Kagame,Yanga katika mchezo wa kirafiki dhidi ya klabu ya African Lyon.Katika mchezo huo ulichezwa kwenye uwanja wa Taifa,Dar es salaam.

Yanga walianza kuhesabu mabao hayo katika dakika ya 8 ambapo mabeki wa African Lyon wakiwa katika harakati za kuokoa mchumo ulioelekezwa langoni kwao walijikuta wakijifunga wenyewe,Hadi mapumziko Yanga walikuwa wanaongoza kwa goli hilo moja.
SHAMTE,KAVUMBAGU,TEGETE na MSUVA
Katika kipindi cha pili cha mchezo huo Yanga walifanya mabadiliko kwa kumtoa Hamis Kiiza na nafasi yake kuchukuliwa na Jerry Tegete.Mabadiliko hayo yalionekana kuisaidia Yanga na ndipo katika dakika ya 54 kiungo mchezeshaji Haruna Niyonzima alipoipatia Yanga bao la pili kwa njia ya mkwaju wa penati baada ya madhambi kufanyika katika lango la African Lyon.Katika dakika ya 72 mshambuliaji mpya chipukizi wa Yanga,Simon Msuva aliipatia Yanga bao la tatu kabla ya Jerry Tegete kukamilisha idadi ya mabao manne katika dakika ya 90 ya mchezo huo.
SIMON MSUVA AKISHANGILIA BAO ALILOFUNGA
Kikosi cha Yanga kilikuwa hivi:

Gazeti La Ijumaa>>Unafiki wa Wema Sepetu na Snura.Kisa ni...!!

http://api.ning.com/files/-xhPZ98Kq7naU4FFcReIiALFoGdWOAilKJUB-w9AWqD8WimuhkfJ-5zodXhv2iPTBKUqpP3pBieSWphQctsTvYvNOdfpYg7x/UZINDUZIWAFILAMUYA8.JPG
WEMA NA SNURA
USHOSTITO wa Wema Sepetu na Snura Mushi uliodumu kwa miezi kadhaa umeraruliwa ukidaiwa kuvunjika kwa kuwa ulikuwa wa kinafiki kutokana na kuvunja kiapo walichokula runingani kuwa hatawaachana, Ijumaa Wikienda limejazwa werawera na wabaya wao.
MTU WA KARIBU ATIRIRIKA
Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho ni mtu wa karibu wa mastaa hao, Wema na Snura walikuwa marafiki vinyonga kwani kila mtu alijua muda siyo mrefu watasalitiana na kuanza kuvujisha siri zao na hicho ndicho kilichotokea.
KISA NI NINI?
Kwa mujibu wa chanzo hicho, Wema alidai kuwa Snura amemsema vibaya kwa ndugu zake na kutangaza kwa wanahabari kuwa amerudiana na mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, jambo ambalo lilimchukiza.
Chanzo kilitiririka kuwa baada ya urafiki huo kuvunjika, Wema alimnyang’anya Snura vitu vyote ambavyo alikuwa amemnunulia na kuanzia hapo mawasiliano baina yao yalikatika.
“Snura ameamua kuvunja kile kiapo alichokula runingani kwa machozi, sasa sijui atapata wapi yale mawigi aliyokuwa akipewa na Wema?,” kilihoji chanzo na kuingia mitini.
SNURA ANASEMAJE?
Alifunguka: “Mimi sijui sababu ya urafiki wetu kuvunjika kwa sababu Wema hajaniambia, angekuwa ni mtu mwenye akili na busara angenieleza.”
NYUMBANI KWA WEMA
Ili kupata mzani wa habari hiyo, Ijumaa Wikienda lilimpigia simu Wema lakini haikupokelewa hivyo likatimba nyumbani kwake ambapo wakiongozwa na Vincent Kigosi ‘Ray’, wasanii hao walitumia nafasi yao kumkashifu mwandishi wetu kwa maneno mabaya yasiyoandikika gazetini, tunayafanyia kazi.

Friday, August 10, 2012

Huyu ndo msanii wa kwanza kusign kwaajiri ya shoo za FIESTA 2012 Bongo...!!

Kila mwaka matamasha makubwa ya Fiesta huwa yanafanyika nchi ikiwa ndo yanaelekea kuanza kwa matamasha hayo ambayo hufanyika nchi.Huyu ndo msanii wa kwanza wa Kibongo kusign kwaajili ya kufanya shoo hizo za FIESTA 2012
SHETTA
Baada ya kusign Shetta aliandika kwenye account yake ya BBM kuwa;

Thursday, August 9, 2012

Video ya Agnes Masogange ya ngono hii hapa...!!Tunaomba radhi kwa watakao kereka nayo.


  • Tunaomba radhi kwa watakao kereka nayo.
  • Kama haikufai usiitazame


Friday, August 3, 2012

Huu ulikuwa ujumbe kwa wale watumiaji wa mtandao wa Twitter wenye nia ya account zao kuwa "VERIFIED"kwenye Twitter..!!


Ngoma mpya ya Dogo Janja ft PNC-Ya moyoni.Download na sikiliza hapa.


Wednesday, August 1, 2012

Mrisho Ngassa asema hajui chochote kuhusu Simba na hatojiunga na timu hiyo..!!


Ngassa ameuzwa Simba kama kiroba cha mchele,Azam hawajaongea na Ngassa pia Ngassa mwenyewe hajaongea na Simba juu ya huu uhamisho. Namnukuu ' mimi sina Taarifa official za kuuzwa Simba,sijafanya mazungumzo na azam pamoja na Simba juu ya uhamisho,kifupi Sitajiunga na Simba ! Nimemaliza kumnukuu Mrisho Ngassa.