Facebook LIKE

Tuesday, November 6, 2012

Huyu ndo mtangazaji anayekuja kwa kasi Bongo mwenye ndoto za kuja kuwa......!!


  •  Ana ndoto za kufika mbali katika utangazaji Bongo
  • Afunguka na kusema anavutiwa na utangazaji wa Big Tiger na Ezden
  • Pia anawakilisha kundi maarufu la WAKACHA
HUYU NDO ABBA MOKO


Abbas Yussuph,21,ana dream ya kuwa Big Tigger wa baadae hapa +255 (Tz) kwenye suala la utangazaji,Abbas maarufu kwa jina la utangazaji ‘’Abba Moko’’ ni mwanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari(DSJ) aki-persue Dipolma in Jornalism,anamapenzi makubwa na suala la utangazaji na kwa sasa anashikilia cheo cha muingizaji sauti ya matangazo ya bush hapo chuoni kwake na kuendesha bush hizo az a hoster, pia ni ripota wa entertainment newz @BarmedasTv ya jijin Mwanza. "Huu ni mwanzo mzuri wa kufikia ndoto zangu za kuwa bonge la mtangazaji na  muendeshaji wa matamasha makubwa hapa Tanzania’’
 Kama ilivyo kwa watu wengi, Abba Moko nae ana mtu anayemuangalia kama kioo chake,’’I have been idolizing one of the hottest presenter in Tanzania, Ezden The Rocker wa Kiss Fm."

Ezden Jumanne"Ezden The Rocker" kushoto

"Napenda anavyohost vipindi vyake na  anavyojiweka kinidhamu akiwa kwenye kipindi",anafunguka Abba. Lakini pia ukitoka nje ya Tz land kuna mtu ambaye Abba anampenda na hapa ni moja kwa moja tunashuka pale kwa Obama Marekani, BET na tunamuangalia jamaa anaejiita Big Tigga ambaye ni mtangazaji na muendeshaji wa vipindi vya BET
BIG TIGGER NA ABBA MOKOPia ukiachilia mbali na suala la utangazaji Abba anapenda sana kuwa muandaaji(producer) wa vipindi mbali mbali pamoja na graphit design.’’Sitaki niwe mtu hasiyejua vitu vingi kwenye fani yangu ya utangazaji kwahiyo napenda sana niwe producer wa vipind na matangazo pamoja na graphit design, kwa hiyo mwakani ntapiga shule kuhusu hizi mambo hapo kwa majiran zetu Kenya na very soon naachia ma program goes by de name’’Freestyle Session’’ ni cha mambo ya freestyle kwa undergroundz wakal ambacho kitakuwa kinarushwa kupitia blog yangu SWAGG ZA KITAA kwahiyo fanz wangu na raia wote get ready 4dat’’, ndivyo alivyomalizia kijana huyo mwenye migogo na swagga za kikaka zaidi.Pia Abba Moko ni member wa kundi la muziki lijulikanalo kama ‘’THE SWITCH’’ linaloundwa na Gyan Bobic,Joshy Joh na Abba Moko mwenyewe na kundi hilo lipo ndani ya kundi maarufu la WAKACHA WARRIORS under Flow Ze Banks ,Cyrill"KAMIKAZE" na Jux Vuitton kwahiyo kwa pamoja wanatengeneza kundi linaloitwa (TSWW)
Kutoka kushoto ni Kricha,Jux,Cyrill,GiggaFlow,AbbaMoko,JoshyJoh na GyanBobic
GYAN BOBIC,ABBA MOKO(katikati)na JOSHY JOH
WAKIWAKILISHA KUNDI LA"THE SWITCH"
Kundi hilo are in de booth ready kwa kupika mkwaju mkali waliomshirikisha Flow,Kricha na C.E.O wao Cyrill Kamikaze,na pia kwa xaxa limeachia tshirt zao zinazojulikana km #TEAM DE SWITCH,fashion on fashion..code on code ambazo zimeonekana kufanya vizur kwa raia wengi na funz wao pia.
T-SHIRTS ZA "TEAM DE SWITCH"

T-SHIRTS ZA #TEAM DE SWITCH PIA ZIPO SOKONI 
KWA WANAOHITAJI T-SHIRTS HIZI WASILIANA KWA NAMBA HII +255654781281 au cheki na Facebook hii>>Abba Moko


Sunday, September 23, 2012

Do you know that this Rapper will quit Rapping in order to be a Pornstar
Mystikal is giving music one last shot — but tells TMZ, if he fails to make another hit on his next album … HE’S TURNING TO PORN.
This is not a joke. Mystikal tells us, he needs to make sure the money keeps coming in … and if there’s one thing he’s good at, it’s having filthy sex. So porn is his plan b.
Which is either crazy … or perfect — because Mystikal served SIX YEARS in prison for sexual battery beginning in 2004 after forcing his hairstylist to perform sex acts on him.
But Mystikal is undeterred, telling us he already has a history in porn — winning an AVN award in 2003 for an adult movie he made (he doesn’t actually have sex in it though).
We asked Mystikal who he’d want to star in his first skin flick, and the rapper said Pinky — adding, “She’s a bad bitch. I would take her down in a second.”
As for whether he’s got the requisite hardware to be a male porn star, Mystikal wouldn’t give an exact size, but said, “I’m definitely the man, the myth, and the legend.”

Huyu ndo msichana ambaye amefananishwa na Kim Kardashian inasemekana ameigiza video ya ngono na rapper Kanye WestSaturday, September 1, 2012

MAKALA:Mbwana Samatta;"Realmadrid walinifuata Kinshasa."(Imeandikwa na Edo Kumwembe)

EDO KUMWEMBE, ALIYEKUWA LUBUMBASHI
NI swali linalowaumiza Watanzania wengi.

Je, Samatta anaweza kuuzwa kwenda kucheza Ulaya?
MBWANA SAMATTA
Watanzania wanatamani kumuona Samatta akiendeleza ndoto zake licha ya sasa kuwa staa wa TP Mazembe.
Wengi wangetamani kumuona akicheza moja kati ya ligi kubwa barani Ulaya, iwe Hispania, England, Ufaransa, Italia au Ujerumani.

Nikiwa na Samatta tukielekea katika sehemu moja ya chakula cha mchana kinachopikwa na Watanzania inayoitwa Parachute, Samatta anaonekana kuwa na hisia zile zile za Watanzania.

"Bado nina kiu ya kucheza Ulaya.

Mimi hapa naona napita kwa sababu natamani sana kukipiga Ulaya.

Najua Watanzania wanachotaka na mimi bado sijabadili msimamo wangu, nikipata nafasi ya kucheza Ulaya tu namlilia Moise Katumbi.

Mtu mwenyewe anaonekana kuwa na huruma kidogo," anasema Samatta huku Thomas Ulimwengu akicheka.

Hili la Katumbi ndilo linaonekana kuwa kikwazo kikubwa katika mazungumzo. Hata Samatta mwenyewe anakiri kwamba Katumbi ni tatizo kubwa kwake kuuzwa Ulaya.

"Nimezungumza na Katumbi kuhusu mimi kucheza Ulaya lakini anaonekana hataki kabisa kusikia habari za mimi kuuzwa.

Kuna wakati aliniambia wazi wazi kwamba timu inayonitaka lazima iilipe Mazembe kiasi cha Euro 10 milioni.

Mimi sina thamani hiyo na wala sidhani kuna mchezaji anayecheza Afrika ana thamani hiyo.

"Nadhani hapo nia yake ni kutoniuza. Eti brother, haiwezekani timu itoe Euro 10 milioni kwa ajili yangu.

Nadhani nikimwambia kuwa nataka kuhama lazima kutakuwa na kasheshe," anasema Samatta huku akicheka.

Hata hivyo, Samatta ananishangaza zaidi anaposema kuwa kuna ofa za kutoka Ulaya zimeshafika mezani kwa Katumbi kwa ajili yake.

Ananishangaza zaidi anaposema kuwa hata wababe wa Hispania, Real Madrid walishatuma maskauti wao wamtazame.

"Katumbi aliwahi kuniambia kuwa maskauti wa Real Madrid walisafiri kuja kunitazama wakati tunacheza na Vita katika Ligi Kuu yetu hapa Congo.

Ilikuwa mechi tuliyocheza Kinshasa, lakini siku ile mimi sikucheza vizuri kwa hiyo sidhani kama walivutiwa au vipi," anasema Samatta.

Pamoja na hali hiyo, Samatta anakiri kwamba ili mchezaji wa Mazembe atimize ndoto zake za kucheza Ulaya ni lazima akubali kuona kipato chake cha pesa kinapungua, labda kama akisajiliwa na timu kubwa barani Ulaya.

"Hata hivyo, braza ukihama Mazembe kwenda Ulaya inabidi uende timu inayoeleweka, kama ukienda timu ya kawaida pato lako litapungua sana kwa sababu Mazembe inalipa posho nzuri kuliko hizo timu za Ulaya.

"Unamuona huyu Kabangu (kiungo wa Mazembe aliyeuzwa kwenda Anderlecht misimu miwili iliyopita) amerudi hapa na ameniambia amerudi kwa sababu hapa wanalipa vizuri kuliko Anderlecht. Yupo hapa nadhani unamuona ameshaongea na Katumbi na ameanza mazoezi.

"Hapa tukishinda mechi kama hizi za kimataifa katika Ligi ya Mabingwa, Katumbi anaweka dola laki tatu mezani (Sh 450 milioni). Tunakuwa watu kama 25 na tunagawana pesa zote hizo.

Sasa kwanini tusiendeshe magari haya? Nadhani kuna klabu za Ulaya hazijafikia posho hizi.

"Hata Katumbi mwenyewe amewahi kuniambia kuwa nikitoka hapa kama naenda Ulaya inabidi niende kucheza timu kubwa iliyo juu ya Mazembe hata kwa mapato."

Kwa fedha alizonazo Katumbi, ambaye pia ni Gavana wa Jimbo la Katanga, huku mara zote akiwa anaonekana katika televisheni akifanya shughuli mbalimbali za Serikali, namuuliza Samatta kama huwa anapata muda wa kuzungumza na Katumbi.

"Huwa ananipigia simu mara nyingi. Lakini mpaka yeye awe na jambo lake au ajisikie. Katumbi ana mambo mengi, mara utasikia yuko Ubelgiji mara kesho asubuhi unamuona Lubumbashi.

Mimi nikimpigia simu haipokelewi, inaita tu. Halafu anaweza kunipigia hata saa nane usiku. Ni mtu mkubwa sana hapa."

Baada ya muda tunaenda Western Union ambapo Samatta anatuma pesa kwa baba yake nyumbani Tanzania.

Ni kiasi kikubwa cha fedha, lakini huo unabakia kuwa utaratibu wake wa kila mwezi.

"Huwa natuma fedha nyumbani kila mwisho wa mwezi.

Ni kitu cha kawaida, Mzee Samatta lazima ajivunie kuwa na mwanaye au vipi braza? Ndiyo maisha yalivyo, tunapata baraka za wazee."

"Hawa wachezaji wa Zambia kina Kalaba, Sunguluma, Sinkala ikifika mwisho wa wiki wanaendesha magari yao kwenda hapo Ndola, si mbali ni mwendo wa saa moja tu, mimi na Thomas (Ulimwengu) inabidi tutume fedha tu nyumbani kwa sababu hatuna uwezo wa kurudi Tanzania mara kwa mara."

Asubuhi ya siku ambayo natakiwa kuondoka inafika. Lakini wote watatu, mimi, Samatta na Ulimwengu tunafunga mabegi.

Wao mabegi yao yanalazimika kusafiri kwa basi kwenda Ndola ambako timu itaweka kambi, lakini wachezaji watasafiri jioni kwenda huko na ndege yao binafsi.

Tunafika mpaka mazoezini kwa ajili ya kuwaacha na kisha nichukue gari la Samatta kupelekwa uwanja wa ndege kuwahi ndege ya saa nne asubuhi.

Tofauti na siku nyingine, safari hii hatupaki ile sehemu ambayo Samatta huwa anapaki gari mazoezini. Hii ni kwa sababu Mfalme Mputu anaweza kutuzuia na nikachelewa kwenda uwanja wa ndege.

Thursday, August 30, 2012

Mbuyu Twite atua rasmi JangwaniMbuyu Twite (mwenye jezi ya njano) 
Twite, Twite, Twite!!!!
Hayo ni maneno ya washabiki wa Yanga walikua wakiimba kumshangilia Twite mara baada ya kutua Uwanja wa Ndege wa mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.
Hakika ilikuwa ni furaha, vifijo na nderemo kwa watu waliofurika kumpokea mchezaji wao mpya Mbuyu Twite. 
Mbuyu Twite akiwa na katibu mkuu wa Yanga, Mwesigwa Selestine
Mchezaji mpya wa kimataifa wa timu ya taifa ta Rwanda ,Mbuyu Twite amewasili leo jijini Dar kutokea nchini Rwanda tayari kujiunga na mabingwa wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati timu ya Young Africans.
Twite aliwsali majira ya saa 10:15 kwa majira ya Afrika Mashariki kwa shirika la ndege la Rwanda Air na kupokelewa na viongozi wa Young Africans na washabiki wengi waliojitokeza kumpokea Uwanja wa ndege wa Mwl JK Nyerere.
Mara baada ya kuwasili mlango wa kutokea watu mashuhuri, Twite alipewa jezi ya Yanga yenye namba 4 mgongoni iiiliyoandikwa jina la Aden Rage, mwenyekiti wa Simba. 
Umati mkubwa ulijitokeza kiasi kilichopelekea Twite kushindwa kutokea mlango wa kawaida wa kupelekea uongozi wa uwanja huo kumuongoza Twite kutokea mlango wa wageni mashuhuri.
Msafara ulianza Uwanja wa ndege wa Mwl JK Nyerere kuelekea makao makuu ya klabu, huku magari yakiwa mengi, pikipiki na wengine wakitembea kwa miguu mpaka makao makuu ya klabu. 
Msafara uliendelea mpaka makao makuu ya klabu, kwa kupitia mtaa wa msimbazi ambapo wapenzi na washabiki wa simba hawakuweza kuamini macho yao mara baada ya kumuona Twite akiwa katika gari ndogo ya Yanga, na washabiki na wanachama wakiwazomea simba na kuwakejeli kwa maneno ya dhihaka.


Umati uliojitokeza kumpokea Mbuyu Twite, Uwanja wa Mwalimu JK Nyerere
Mara baada ya kufika makao makuu ya klabu ya Yanga, mchezaji Mbuyu Twite alipanda juu ghrorofani kuwasalimia washabiki na wanachama waliojitokeza kumpokea, kisha alikabidhiwa funguo ya chumba ambacho atakua akikitumia kwa kipindi chote atakachokuwa Yanga.
Mbuyu Twite amesema anajisikia vizuri, na furaha na mwenye bahati kuja kuchezea timu ya Yanga na anawaahidi kuonyesha kiwango cha juu kipindi chake chote atakaoitumikia Young Africans, Twite kesho anatajumuika na wenzake katika mazoezi asubuhi Uwanja wa Loyola kabla ya jumamosi kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Coastal Union.

Wednesday, August 29, 2012

Magoli ya mechi ya RealMadrid dhidi ya Barcelona haya hapa kama ulikosa mechi RealMadrid 2-1 Barcelona

Hili ni Goli la kwanza lililofungwa na Gonzalo Higuain wa RealMadrid

Gonzalo HiguaĆ­n goal(Real Madrid vs Barca 2nd leg supercup)Twitter @TheKSTYLES from Kelly Kelvin
on Vimeo.
Hili ndilo goli alilofunga Cristiano Ronaldo ambalo limeiwezesha RealMadrid kubeba kombe la kwanza msimu huu ni kombe la SuperCup linalokutanisha bingwa wa LIGI(RealMadrid) na bingwa wa KOMBE LA MFALME(Barcelona).Mechi ya kwanza Barca walishinda 3-2 nyumbani kwao ila ugenini wamefungwa 2-1 kwahiyo RealMadrid wamebeba kombe hilo kwa faida ya mabao ya ugenini

Real Madrid Vs Barcelona 2-1 Cristiano Ronaldo Fantastic Goal Spanish Super Cup 29-082012 (2nd leg)Twitter @TheKSTYLES from Kelly Kelvin on Vimeo.
HIGHLIGHTS ZA MABAO YOTE HII HAPA

2-1 Real Madrid highlights win its ninth Supercup Twitter @TheKSTYLES from Kelly Kelvin on Vimeo.