Facebook LIKE

Showing posts with label Yanga. Show all posts
Showing posts with label Yanga. Show all posts

Thursday, August 30, 2012

Mbuyu Twite atua rasmi Jangwani



Mbuyu Twite (mwenye jezi ya njano) 
Twite, Twite, Twite!!!!
Hayo ni maneno ya washabiki wa Yanga walikua wakiimba kumshangilia Twite mara baada ya kutua Uwanja wa Ndege wa mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.
Hakika ilikuwa ni furaha, vifijo na nderemo kwa watu waliofurika kumpokea mchezaji wao mpya Mbuyu Twite. 
Mbuyu Twite akiwa na katibu mkuu wa Yanga, Mwesigwa Selestine
Mchezaji mpya wa kimataifa wa timu ya taifa ta Rwanda ,Mbuyu Twite amewasili leo jijini Dar kutokea nchini Rwanda tayari kujiunga na mabingwa wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati timu ya Young Africans.
Twite aliwsali majira ya saa 10:15 kwa majira ya Afrika Mashariki kwa shirika la ndege la Rwanda Air na kupokelewa na viongozi wa Young Africans na washabiki wengi waliojitokeza kumpokea Uwanja wa ndege wa Mwl JK Nyerere.
Mara baada ya kuwasili mlango wa kutokea watu mashuhuri, Twite alipewa jezi ya Yanga yenye namba 4 mgongoni iiiliyoandikwa jina la Aden Rage, mwenyekiti wa Simba. 
Umati mkubwa ulijitokeza kiasi kilichopelekea Twite kushindwa kutokea mlango wa kawaida wa kupelekea uongozi wa uwanja huo kumuongoza Twite kutokea mlango wa wageni mashuhuri.
Msafara ulianza Uwanja wa ndege wa Mwl JK Nyerere kuelekea makao makuu ya klabu, huku magari yakiwa mengi, pikipiki na wengine wakitembea kwa miguu mpaka makao makuu ya klabu. 
Msafara uliendelea mpaka makao makuu ya klabu, kwa kupitia mtaa wa msimbazi ambapo wapenzi na washabiki wa simba hawakuweza kuamini macho yao mara baada ya kumuona Twite akiwa katika gari ndogo ya Yanga, na washabiki na wanachama wakiwazomea simba na kuwakejeli kwa maneno ya dhihaka.


Umati uliojitokeza kumpokea Mbuyu Twite, Uwanja wa Mwalimu JK Nyerere
Mara baada ya kufika makao makuu ya klabu ya Yanga, mchezaji Mbuyu Twite alipanda juu ghrorofani kuwasalimia washabiki na wanachama waliojitokeza kumpokea, kisha alikabidhiwa funguo ya chumba ambacho atakua akikitumia kwa kipindi chote atakachokuwa Yanga.
Mbuyu Twite amesema anajisikia vizuri, na furaha na mwenye bahati kuja kuchezea timu ya Yanga na anawaahidi kuonyesha kiwango cha juu kipindi chake chote atakaoitumikia Young Africans, Twite kesho anatajumuika na wenzake katika mazoezi asubuhi Uwanja wa Loyola kabla ya jumamosi kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Coastal Union.

Monday, August 20, 2012

Yanga yaichakaza African Lyon katika Uwanja wa Taifa....!!


KIKOSI CHA YANGA DHIDI YA AFRICAN LYON
Mabao yaliyowekwa wavuni na Haruna Niyonzima,Simon Msuva,Jerry Tegete na moja la kujifunga yalitosha kuipa ushindi wa mabao 4-0,Mabingwa wa Kombe la Kagame,Yanga katika mchezo wa kirafiki dhidi ya klabu ya African Lyon.Katika mchezo huo ulichezwa kwenye uwanja wa Taifa,Dar es salaam.

Yanga walianza kuhesabu mabao hayo katika dakika ya 8 ambapo mabeki wa African Lyon wakiwa katika harakati za kuokoa mchumo ulioelekezwa langoni kwao walijikuta wakijifunga wenyewe,Hadi mapumziko Yanga walikuwa wanaongoza kwa goli hilo moja.
SHAMTE,KAVUMBAGU,TEGETE na MSUVA
Katika kipindi cha pili cha mchezo huo Yanga walifanya mabadiliko kwa kumtoa Hamis Kiiza na nafasi yake kuchukuliwa na Jerry Tegete.Mabadiliko hayo yalionekana kuisaidia Yanga na ndipo katika dakika ya 54 kiungo mchezeshaji Haruna Niyonzima alipoipatia Yanga bao la pili kwa njia ya mkwaju wa penati baada ya madhambi kufanyika katika lango la African Lyon.Katika dakika ya 72 mshambuliaji mpya chipukizi wa Yanga,Simon Msuva aliipatia Yanga bao la tatu kabla ya Jerry Tegete kukamilisha idadi ya mabao manne katika dakika ya 90 ya mchezo huo.
SIMON MSUVA AKISHANGILIA BAO ALILOFUNGA
Kikosi cha Yanga kilikuwa hivi:

Wednesday, August 1, 2012

Mrisho Ngassa asema hajui chochote kuhusu Simba na hatojiunga na timu hiyo..!!


Ngassa ameuzwa Simba kama kiroba cha mchele,Azam hawajaongea na Ngassa pia Ngassa mwenyewe hajaongea na Simba juu ya huu uhamisho. Namnukuu ' mimi sina Taarifa official za kuuzwa Simba,sijafanya mazungumzo na azam pamoja na Simba juu ya uhamisho,kifupi Sitajiunga na Simba ! Nimemaliza kumnukuu Mrisho Ngassa.

Tuesday, July 17, 2012

Yanga yafanya mauaji Kagame yawapiga Wasudan goli 7


Mabao yaliyotiwa kimiani na washambuliaji Mganda Hamis Kiiza,Said Bahanuzi na kiungo Nizar Khalfan yameiwezesha klabu ya Yanga kuibuka na ushindi wa goli 7-1 dhidi ya timu ya Waw Salaam ya Sudan.

Katika mchezo huo ulitawaliwa zaidi na Yanga mshambuliaji Said Bahanuzi ndiye aliyeipatia Yanga bao la kuongoza katika dakika ya 12.Dakika tano baadae Bahanuzi tena alitumbukiza mpira kimiani na kuipatia Yanga bao la pili katika dakika ya 17.Mshambuliaji Mganda Hamis Kiiza alianza kuhesabu mabao yake manne aliyofunga katika pambano hilo katika dakika ya 18,25,30 na 35.Hadi timu hizo zinaenda mapumziko Yanga walikuwa mbele kwa mabao 6-0.

Katika kipindi cha pili Yanga waliwatoa Kevin Yondan,Haruna Niyonzima na Stephano Mwasika na nafasi zao kuchukuliwa na Juma Seif,Rashid Gumbo na Idrissa Rashid.Katika dakika ya 75 kiungo Nizar Khalfan aliipatia Yanga bao la saba.Waw Salaam walijipatia bao lao katika dakika ya 90 ya mchezo

Katika mchezo huo kikosi cha Yanga kilikuwa hivi;

Sunday, July 15, 2012

Manji mwenyekiti mpya wa klabu ya Yanga,matokeo yote ya uchaguzi mdogo Yanga haya hapa

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa Klabu ya Yanga, Jaji John Mkwawa
 kushoto akiwa na Mjumbe wa kamati hiyo Mzee Mzimba



Yusuf Manji amechaguliwa kuwa mwenyekiti mpya wa klabu ya Young Africans Sports Club, uchaguzi ulioitishwa kujaza nafasi zilizoachwa wazi, kufuatia kujiuzuru kwa baadhi ya wajumbe wa kamati ya utendaji, mwenyekiti na makamu wake.
Akitangaza matokeo hayo, majira ya saa 10:30 alfajiri katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wa klabu ya Yanga Jaji John Mkwawa amemtangza Manji kama mishindi wa nafasi ya uenyekiti kufuatia kupata asilimia 97% ya kura zote zilizopigwa katika nafasi hiyo.
Nafasi ya Makamu Mwenyekiti imekwenda kwa Clement Sanga aliyejipatia asilimia 62% ya kura zote zilizopigwa katika nafasi ya u makamu mwenyekiti.
Abdallah Bin Kleb, Moses Katabaro, Aaron Nyanda na George Manyama  wamechaguliwa katika nafasi ya ujumbe wa kamati ya  Utendaji.
Jaji Mkwawa amewashukuru wana Yanga kwa kuwa wastaarabu na watulivu, kitu kilicholekea kufanyika uchaguzi kwa amani na zoezi hilo kumalizika salama pasipo kuwa na rabsha yoyote.
Matokeo kamili ya wagombea ni:

Nafasi ya Mwenyekiti:
Yusuf Manji (kura 1876)  97.0%,  John Jembele (kura 40) 2.6%, Edgar Chibura (kura 4) 0.24%

Nafasi ya Makamu Mwenyekiti:
Clement Sanga (kura 1948) 62.6%, Yono S Kevela (kura 475) 23%, Ayoub Nyenzi (kura 288) 14%

Nafasi ya Ujumbe:
Abdallah Bin Kleb (kura 1942),Moses Katabaro (kura 1068),Aaron Nyanda (kura 922), Geroge Manyama (kura 682), Beda Tindwa (kura 391), Edgar Fongo (kura 295), Graticius Ishengoma  (kura 247), Jumanne Mwamenywa (kura 251), Justine Baruti (610), Lameck Nyambaya (kura 425), Omary Ndula (kura 170), Peter Haule (441), Ramadhan Said (249), Yono Kivela (123)

Kutokana na matokeo yalivyo hapo juu safu ya viongozi waliochaguliwa ni:
Mwenyekiti: Yusuf Manji,
Makamu Mwenyekiti: Clement Sanga
Wajumbe: Abdallah Bin Kleb, Moses Katabaro, Aaaron Nyanda, Geroge Manyama 

Thursday, July 12, 2012

Kikosi cha Yanga kitakachoshiriki michuano ya Kagame hiki hapa....!

KOCHA wa Yanga, Mbelgiji Tom Saintfiet amewaacha kwenye kikosi kitakachoshiriki michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame kuanzia Jumamosi wachezaji watatu nyota na chipukizi, Omega Seme, Simon Msuva na Frank Damayo kwa sababu watakuwa na majukumu ya kitaifa kwa muda mrefu.
 
Akizungumza na Waandishi wa Habari mchana huu, makao makuu ya klabu makutano ya Mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam, Saintfiet alisema kwamba wachezaji hao watakuwa na timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, inayojiandaa mechi ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika Julai 29 dhidi ya Nigeria.
 
“Kwa  mujibu wa kanuni natakiwa kuwaachia wachezaji siku tano kabla ya mechi, na Jumamosi wanacheza na Rwanda, Jumatatu wanarudiana na Rwanda, baada ya hapo watakuwa kwenye maandalizi ya mechi na Nigeria, kwa hivyo sitakuwa nao hata kwenye Nusu Fainali, kwa sababu hiyo nimeamua kuwaacha,”alisema.
 
Saintfiet alisema amemtema pia Nahodha wa klabu hiyo, Nsajigwa Shadrack katika kikosi cha wachezaji 20, lakini amesema mchezaji huyo ni muhimu na atakuwa naye kwenye Ligi Kuu.
 
Amewataja wachezaji aliowateua baada ya kushauriana na wasaidizi wake, Freddy Felix Minziro na Mfaume Athumani kuwa ni;
 
KIKOSI CHA YANGA KAGAME;

Tuesday, July 10, 2012

Yanga yaichapa JKT Ruvu kuelekea michuano ya Kagame

Mabingwa wazamani wa Tanzania,Dar Young Africans wameichapa timu ya JKT Ruvu 2-0 katika mchezo wa kirafiki uliochezwa leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.Ukiwa na mchezo wa kwanza wa kirafiki kwa kocha mpya wa klabu hiyo Mbeligiji,Tom Saintfiet.

Yanga ambayo inajiandaa na michuano ya Kagame ambayo inaanza wikiendi hii walijipatia mabao yake kupitia beki wake kisiki wa kati,Nadir Haroub"Cannavaro" katika dakika ya 18.Hadi mchezo huo unaenda mapumziko Yanga walikuwa mbele kwa bao hilo moja.Katika kipindi cha pili Yanga walifanya mabadiliko kwa kumtoa kiungo Nizar Khalfan na nafasi yake kuchukuliwa na mshambuliaji mganda Hamis Kiiza,ambaye katika dakika ya 73 ya mchezo huo aliipatia Yanga bao la pili.

Katika pambano hilo Kikosi cha Yanga kilikuwa hivi;

Wednesday, July 4, 2012

Kocha mpya wa Yanga awasili.........!Huyu hapa

Photo: kocha yanga...
ALIPOWASILI UWANJA WA NDEGE WA JK NYERERE AKIWA NA BAADHI YA VIONGOZI MASHABIKI NA WANACHAMA WA YANGA MARA BAADA YA KUWASILI










Saturday, June 30, 2012

Yanga yaichapa Express ya Uganda katika mechi ya kirafiki kuelekea michuano ya Kagame pia yatangaza walioachwa rasmi.

Yanga imewachapa Mabingwa wa Uganda,Express FC katika mchezo wa kirafiki uliochezwa leo katika Uwanja wa Taifa,Dar es salaam.Katika mchezo huo mabao ya Yanga yalitiwa kimiani na mshambuliaji Jerry Tegete katika dakika ya 3 na 19.
Kikosi cha Yanga kilikuwa hivi;

Thursday, June 21, 2012

Nurdin Bakary huyoo Azam huku Yanga wakimrejesha kundini winga wao wa zamani......!

Yanga wameendelea kuonyesha mabavu katika usajili baada ya kumsajili Kelvin Yondani, Nizar Khalfan, Barthez, Domayo na wengine wengi, leo taarifa za usajili kutoka klabu hiyo zinasema kwamba klabu hiyo ipo kwenye mazungumzo na klabu ya Azam ili kuweza kumsajili winga wa kimataifa wa Tanzania Mrisho Khalfan Ngassa.


Habari za ndani zinadai kwamba zinadai kwamba Ngassa, Yanga na Azam wapo kwenye mazungumzo ya mwisho na huenda kesho kutakuwa na habari nzuri kwa wapenzi wa Yanga juu ya kurudi kwa kipenzi chao Ngassa mitaa ya Jangwani.

Katika usajili huo Yanga wapo tayari kulipa kiasi kikubwa cha fedha na kumtoa kiungo Nurdin Bakary ili kuweza kumtwaa winga huyo ambaye alishwahi kuichezea Yanga kwa mafanikio kalba ya kuhama kwa uhamisho uliovunja rekodi ya ndani ya usajili baada ya Azam kulipa milioni 60 kwa Yanga na kumtwaa Ngassa

Wednesday, June 20, 2012

Bahanuzi,Barthez,Abdul na Nizar kivutio kwa mashabiki wa Yanga leo Kaunda......!

Kikosi cha Mabingwa wa soka wa Afrika Mashariki na Kati, kimeendelea na mazoezi leo katika Uwanja wa Kaunda jijini Dar es Salaam,huku miongoni mwa wachezaji waliosajiliwa msimu huu tayari wakiwa wamejiunga katika mazoezi hayo.
Katika mazoezi hayo aliyekuwa golikipa wa timu ya Simba Mustapha Ally Barthez, mshambuliaji wa timu ya Mtibwa Sugar ya Morogoro Said Bahanuzi na beki wa kulia wa timu hiyo ya Mtibwa Juma Abdul walichangamsha mazoezi hayo yaliyokuwa yakisimamiwa na Fred Felix pamoja na kocha wa magolikipa Mfaume Athuman.
 Wachezaji wengine walioshiriki katika mazoezi hayo ni Oscar Joshua,Stephano Mwasika,Nadir Haroub,Ibrahim Job,Juma Seif,Shamte Ally na Athumani Idd Chuji, wachezaji wengine ni Omega Seme,Jerryson Tegete,Idrisa Rashid,Godfrey Taita,Nizar Khalifan,Hamis Kiiza na Kenneth Asamoah.
Wakati huo huo Kocha Fred Minziro amesema amefurahi kuona kikosi chake kikizidi kuimarika baada ya wachezaji wengi kujiunga katika mazoezi hayo.



Tuesday, June 19, 2012

Picha za baadhi ya wachezaji walioanza kuwasili leo YANGA hizi hapa,Mwape nae ndani angalia hapa...!!


Mshambuliaji Mzambia, Davies Mwape ambaye imeelezwa ameachwa Yanga, akiwa makao makuu ya klabu hiyo makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam baada ua kuwasili leo kutoka kwao, tayari kuanza mazoezi. Je, nini hatima yake
Beki Ibrahim Job akiwa na mwanachama wa klabu hiyo
Kocha wa makipa Mfaume Athumani kulia akiwa Kaimu Kocha Mkuu, Freddy Felix Minziro leo Jangwani.
NDANI YA GHETTO; Chumbani kutoka kulia ni Godfrey Taita, Julius Mrope, Nadir Haroub 'Cannavaro' na Stefano Mwasyika aliyeipa kisogo kamera.


Pius Kisambale

Monday, June 18, 2012

Yanga yarundika mabeki wa kati,wengine waingiwa na hofu ya nafasi zao katika kikosi hicho pia hofu kama hiyo yatanda katika nafasi ya ushambuliaji na kiungo........!


BAADHI ya wachezaji wa Yanga wanaocheza nafasi ya beki wa kati namba nne na tano wameanza kuingiwa na mchecheto wa kupata namba katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo kutokana na uongozi kuendelea kusajili wachezaji wanaocheza nafasi hizo.

Hali hiyo imekuja hivi karibuni baada ya klabu hiyo kuwanasa mabeki wawili, Kelvin Yondani kutoka Simba na Ladislaus Mbogo wa Toto Africa.

Usajili wa wachezaji hao unaifanya Yanga kufikisha wachezaji nane ambao ni Chacha Marwa, Nadir Haroub 'Cannavaro', Athumani Idd 'Chuji',Ibrahim Job, Zubery Ubwa, Bakari Mbegu, Yondani pamoja na Mbogo.

Wakizungumza na gazeti la Mwananchi kwa nyakati tofauti hivi karibuni, baadhi ya wachezaji hao (majina tunayo MwananchiCoLtd) walionekana kuwa na hofu ya kupata namba katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo.Hata hivyo msimu uliopita waliokuwa wanaanza katika kikosi cha kwanza walikuwa Nadir Haroub na Athumani Iddi

Walisema kwa sasa wanachosubiri ni timu kuingia kambini kujiandaa na michuano ya Kagame na huko ndipo watakapopata majibu sahihi ya maswali yao.

"Siwezi kuzunguza lolote kwa sasa juu ya hali hiyo kwa sababu mimi siyo kocha lakini majibu yatajulikana baada ya kuingia kambini hivi karibuni."

Kikosi hicho cha Yanga kinatarajia kuingia kambini leo kujiandaa na harakati zake za kutetea ubingwa wa mashindano ya Kagame ikiwa ni pamoja na mikikimikiki ya msimu ujao wa Ligi Kuu.

Yanga wakiwa mazoezini leo tarehe 18/06/2012 chini ya Kocha Msaidizi Fred F Minziro
Hata hivyo kuna taarifa kuwa baadhi ya mabeki hao wataachwa na Timu hiyo ya Mitaa ya Twiga na Jangwani.

Thursday, June 7, 2012

Baada ya Yondan sasa Yanga yafanya kufuru nyingine sasa kumchukua mfungaji bora wa CECAFA,Simba waja juu.....!

Baada ya Yanga kutangaza kumsajiri Kelvin Yondan kwa kitita cha shillingi millioni30 sasa klabu hiyo imekamilisha taratibu za kumsajili kipa ya Wekundu hao Ally Mustapha"Barthez" kipa huyo inasemekana anakwenda Jangwani kuziba pengo la Mghana Yaw Berko ambaye inasemekana ameachwa na klabu hiyo yeye pamoja na Mghana mwenzake mshambuliaji Kenneth Asamoah.Katika hatua nyingine pia inasemekana Yanga inataka kuipiku Simba katika mbio za kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Simba pamoja na AFC,Danny Mrwanda pamoja na beki Juma Nyosso ila kumeibuka sitofahamu kwa beki huyo ambapo baadhi ya wadau wa klabu hiyo wanadai beki huyo ni Simba damu hivyo wanahofia hujuma.Pia kuna habari kuwa Yanga wanafanya taratibu za kubadilishana wachezaji na Mtibwa ambapo itawalazimu Yanga wamwachie kipa Shaban H Kado arejee Mtibwa kwa makubaliano ya kubadilishana na wachezaji beki chipukizi wa kulia,Juma Abdul ambaye anajiunga na timu hiyo kuziba pengo la Shadrack Nsajigwa ambaye anaachwa na Yanga pamoja na mshambuliaji Said Bahanuzi au Hussein Javu.Na katika kuhakikisha wanaziba mapengo ya wachezaji Kenneth Asamoah na Davies Mwape ambao wameachwa Yanga inasemekana wanamfuatilia kwa karibu mfungaji bora wa michuano ya Cecafa2011 Mrwanda Meddie Kagere,huku viongozi wa Yanga wakikili kumkosa kiungo Mganda Owen Kasule anayekwenda El Merreikh ya Sudan.Kwa taarifa fupi ni kwamba hadi sasa Yanga imekamilisha usajili wa wachezaji beki wa kushoto David Luhende kutoka Kagera,Juma Abdul wa Mtibwa,Nizar Khalfan aliyekuwa anacheza soka la kulipwa Marekani na beki Kelvin Yondan aliyekua Simba ila uongozi wa Simba umeujia juu usajili huo kwa madai Yondan anamkataba na Simba wa miaka miwili ila beki huyo inasemekana amekana kwamba hana mkataba na Simba na yeye ni mchezaji halali wa Yanga.Na walioachwa ni Shadrack Nsajigwa,Davies Mwape,Kenneth Asamoah,Bakary Mbegu,Zuber Ubwa,Abuu Ubwa na Kiggi Makaasy anayekwenda Simba..Huku usajili huo wa Yanga ukifanywa Timu ikiwa haina kocha hata msaidizi...!!!!Usajili chini ya Kocha mkuu Yussuph Manji na wasadizi wake Seif Ahmed"Magari" na Ahmed Bin Kleb.BREAKING NEWS ni kwamba pia Yanga wanamfutilia kiungo mkongwe Shaban Nditi ila kuna taarifa kuwa kiungo huyo amejiunga na Coastal Union.

Tuesday, May 29, 2012

Tetesi za Usajili Bongo hizi hapa,Unaijua bei ya kumng'oa Okwi Msimbazi..?Hii hapa........

1.Golikipa Mghana wa Yanga kubaki Jangwani mara baada ya kuongeza mkataba na klabu hiyo ya Yanga.

2.Imefahamika kuwa kiungo wa zamani wa klabu ya VancouverWhiteCaps,NizarKhalfan ameitosa klabu ya Simba na kuamua kujiunga na mabingwa wa zamani Yanga,pia inasemekana amesaini mkataba wa mwaka mmoja na Yanga.

3.Simba yaachana na JerryTegete,klabu ya Simba imesitisha mpango wake wa kumsajili mshambuliaji wa Yanga JerryTegete baada ya kusemekana kuwa mchezaji huyo ana mapenzi zaidi na Yanga hivyo wana wasiwasi kama ataweza kuitumikia Simba vizuri.

4.Yanga kuibomoa MtibwaSugar,klabu ya Yanga ipo kwenye hatua ya kuwasajili wachezaji watatu kutoka Mtibwa kwa mpigo.Wachezaji hao ni washambuliaji SaidiBahanuzi na HusseinJavu pamoja na beki wa kulia chipukizi JumaAbdul.Pia inasemekana Yanga itajaribu kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Simba,DannyMrwanda ila kama itashindikana wataelekeza nguvu zao kwa Javu na Bahanuzi.

5.Shiboli asaini PolisiMorogoro inaelezwa kuwa mshambuliaji wa zamani wa Simba,KageraSugar amesaini na timu ya PolisiMorogoro baada ya kuachwa na CoastalUnion.

6.RamadhaniChombo"Redondo";Siondoki Azam FC,kiungo mchezeshaji wa Azam RamadhaniChombo amesema hatarajii kuondoka katika klabu hiyo huku akisema Azam mwakani itashiriki michuano ya CAF.

7.Simba yataja bei ya EmmanuelOkwi,Yanga yadai wanataka kumng'oa Msimbazi mshambuliaji huyo raia wa Uganda.Simba wasema ni dola 900000 zaidi ya bilioni moja za kitanzania

8.Azam FC;Tulishakamilisha usajili wetu msituhusishe na kusajili wachezaji wengine.

9.Coastal union;Usajili tuliofanya lazima tuchukue ubingwa msimuu ujao.Wasema lazima wacheze michuano ya kimataifa na kuiwakilisha nchi kimataifa,wazionya Simba na Yanga.

Sunday, May 27, 2012

Hii ndio gari anayomiliki mchezaji wa klabu ya Yanga,Shaban Kado.

Golikipa ya Yanga Shaban Kado hivi karibuni aliweka kwenye mtandao wa kijamii wa facebook gari yake ambayo anaimiliki.