Facebook LIKE

Saturday, June 30, 2012

Yanga yaichapa Express ya Uganda katika mechi ya kirafiki kuelekea michuano ya Kagame pia yatangaza walioachwa rasmi.

Yanga imewachapa Mabingwa wa Uganda,Express FC katika mchezo wa kirafiki uliochezwa leo katika Uwanja wa Taifa,Dar es salaam.Katika mchezo huo mabao ya Yanga yalitiwa kimiani na mshambuliaji Jerry Tegete katika dakika ya 3 na 19.
Kikosi cha Yanga kilikuwa hivi;
Ally Mustapha,Juma Abdul,Oscar Joshua/Stephano Mwasika,Nadir Haroub,Kelvin Yondan/Ladislaus Mbogo,Athumani Iddi,Simon Msuva/Idrissa Rashid,Frank Domayo,Jerry Tegete/Hamis Kiiza,Said Bahanuzi/Omega Seme,Nizar Khalfan/Shamte Ally


Katika hatua nyingine Young Africans Sports Club imewasilisha jumla ya majina 13 ya wachezaji ambao imeachana nao mwishoni mwa msimu ulioisha kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF.
Wachezaji waliomaliza mikataba yao ni:
1.Godfrey Bonny
2.Kiggi Makasi
3.Abuu Ubwa
4.Bakari Mbega
5.Chacha Marwa
6.Atif Amour

Wachezaji ambao klabu imeamua kuvunja nao mikataba ni:
1.Davies Mwape
2.Kenneth Asamoah
3.Julius Mrope
4.Iddi Mbaga
5.Zuberi Ubwa
6.Pius Kisambale
NB: Shaban Hassan Kado ametolewa kwa mkopo kwenda timu ya Mtibwa Sugar 

No comments:

Post a Comment