Facebook LIKE

Monday, June 18, 2012

Edo Kumwembe:Lazima tucheze michuano ya Kimataifa mwakani kama sio Mabingwa basi nafasi ya pili yetu,aanika bunduki zao mpya yupo muuaji aliyefunga kila mechi raundi ya pili ya Ligi Kuu

UONGOZI wa klabu ya Coastal Union ya Tanga umetangaza wachezaji wanane iliyowasajili kwa ajili ya kuichezea timu msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

Msemaji wa timu hiyo, Edo Kumwembe aliwataja wanandinga hao kuwa ni Razak Khalfan na Seleman Kassim waliotokea African Lyon, Sudi Mohamed (Toto African), Nsa Job (Villa Squad) Othman Omar (Oljoro), Atupele Green (Yanga), Jackson Chove (huru) na Juma Mpongo aliyekuwa anacheza soka ya Burundi.

"Kimsingi usajili wetu kwa wachezaji wa ndani umekalika na hatutachukua mchezaji mwingine hapa nyumbani," alisema Kumwembe.

Aliongeza  kuwa, kwa upande wa nyota wa kigeni klabu yake ina mpango wa kusajili wachezaji wawili pekee  katika nafasi ya kuingo mkabaji na beki wa kati.

"Kwa ujumla tumejipanga kufanya mambo makubwa msimu ujao, hatutaki bla bla tena," alisema Kumwembe.

Pia, alisema mshambuliaji wao, Benard Mwalala hatakuwepo kwenye kikosi hicho msimu ujao baada ya kuomba aachwe ili akacheze soka ya kulipwa Arabuni

Edo pia alitoa tahadhari kwa timu zingine zinazoshiriki Ligi Kuu ya TZ kuwa msimu huu ni wao na kila atakae kuja mbele yao ni kichapo hii ni katika kuhakikisha wanashika nafasi mbili za juu.

No comments:

Post a Comment