Facebook LIKE

Monday, June 25, 2012

Baada ya Dogo Janja sasa ni rapper Suma Mnazaleti


Rapper Suma Mnazaleti ametangaza kujiunga na Dogo Janja kwenye
list ya wasanii waliochini ya uongozi wa kundi la WATANASHATI lililomrudisha Dogo Janja kutoka Arusha wiki iliyopita.
Suma amesema “sababu iliyonifanya niingie Watanashati ni kwamba nimekaa nje ya uongozi kwa muda wangu wote wa Muziki kwa zaidi ya miaka mitatu, nimekua ni mtu ambae nafanya maamuzi mwenyewe kuanzia kwenye kurekodi nyimbo mpaka kusimamia kazi zangu bila usimamizi wa mtu mwingine, hilo ndio naona limekua likinicheleweshea malengo yangu niliyoyapanga kwenye muziki”
SUMA MNAZALETI
“Mimi ndio niliwafata WATANASHATI kwa sababu nilishajifunza kwamba niko kwenye kutafuta maisha na kutafuta inabidi ujue hata kama una vyeti inabidi upeleke vyeti vyako ofisini ili uajiriwe so mimi ndio nikamtafuta meneja Ostaz Juma”(habari kwa hisani ya millardayo.com)

No comments:

Post a Comment