Facebook LIKE

Friday, June 1, 2012

ChidBenz,Madee wajibu mapigo kwa disi za Ney wa Mitego

Picha kwa hisani ya millardayo.com
Wasanii ChidBenz pamoja na Madee wamejibu mapigo kwa msanii,Ney wa Mitego ambaye aliwadisi wasanii hao katika ngoma yake.Wakizungumza katika kipindi cha XXL cha CloudsFM wakali hao kutoka Ilala na Manzese.ChidBenz alidai kuwa hamtambui msanii Ney wa Mitego na hajawahi kumsikia,pia alisema msanii huyo anatafuta njia ya kutokea kupitia majina ya wasanii na watu maarufu pia alisema kama kungekuwa na msanii kama huyo basi angekuwa ameshafanya nae kazi kwani alidai kuwa tayari amefanya kazi na wasanii wote wakali wa bongo.Kwa upande wa raisi wa Manzese,Madee amesema nikawaida kwa mtu ambaye hajulikani kutaka kupata au kuteka hisia za watu kupitia majina ya watu maarufu.Msanii Ney wa Mitego alimdisi ChidBenz kwa kitendo chake cha kutoboa pua huku pia akimdisi Madee kuwa hawezi kuwa raisi wa Manzese pia akasema katika ngoma yake kuwa Madee ahamishie malumbano yake na AfandeSele katika Taarabu hayo yote yapo kwenye ngoma ya Ney wa Mitego.

No comments:

Post a Comment