Kiongozi wa Usajili wa Yanga, Seif Ahmed
aliliambia gazeti la Mwanaspoti jana kwamba: "Yanga haijamsajili Ngassa kutoka
Azam wala Nurdin haendi kokote.
"Nisikilize, mimi ndiye ninayesimamia usajili wote wa Yanga. Tunaheshimu mkataba wa Ngassa na Azam na hata kama angekuwa hana mkataba, tungemsajili kama tungemhitaji na si yeye atuhitaji sisi. Ndivyo tufanyavyo usajili siku zote, hatuwezi kusajili ilimradi, tunazingatia nafasi na matakwa ya benchi la ufundi.
"Mimi kukutana na Ngassa mtaani haimaanishi kwamba tunataka kumsajili ni rafiki yangu haihusiani na mambo ya Yanga. Huu ni mpira siyo siasa, hakuna nafasi ya Ngassa kwa sasa waambieni watu waelewe."
Katika hatua nyingine Yanga inatarajia kumtangaza kocha mpya siku ya Jumatatu,ila kuna tetesi kocha huyo akawa ni Mkenya Jacob Ghost Mulee ambaye pia inasemekana imeiambia Yanga kama wanataka kumpa Timu basi wahakikishe wanampa mkataba wa mwaka mmoja na kuendelea sio mkataba wa muda mfupi kama Yanga walivyopanga kumpa.Yanga wanataka kumpa mkataba wa miezi miwili tu ya kuinoa timu katika mashindano ya Kagame.

No comments:
Post a Comment