Facebook LIKE

Tuesday, June 26, 2012

Makombora ya Said Bahanuzi yawachanganya mashabiki ya Yanga mazoezini


  • Dumayo,Abdul,Msuva,Mbogo nao wapagawisha mashabiki Kaunda
  • Niyonzima nae kutua kuongeza kachumbari
  • Minziro achanganyikiwa hajui ampange nani amwache nani?
  • Straika Mnyarwanda nae kuvaa jezi za njano na kijani
Vifaa vipya vilivyosajiliwa msimu huu vinazidi kuwapa kiwewe wapenzi na mashabiki wa klabu ya Yanga huku kocha msaidizi Fred Felix Minziro akiwa na kibarua kigumu cha kutambua vipaji vya kila mchezaji ambapo kila mmoja akionyesha jitihada za kutafuta namba ya kudumu .
Katika mazoezi hayo mchezaji Said Bahanunzi
alionyesha utaalamu wake wa kuachia makombora ya masafa marefu huku akishangiliwa mara kwa mara  na mashabiki waliokuwa wakishuhudia mazoezi katika uwanja wa Kaunda jijini Dar es Salaam.
Wachezaji wengine wapya waliokuwa wakionyesha vitu vyao ni pamoja na Juma Abdul, Charles Domayo kaka wa Frank Domayo, Saimon Msuva pamoja na Ladislaus Mbogo ambao mara kwa mara walikuwa wakionyesha vipaji vyao vya kusakata soka.
WACHEZAJI WA YANGA WAKIWA MAZOEZINI

Kwa upande wa magolikipa waliokuwa wakiteseka na makombora hayo ni pamoja na Ally Mustapha "Barthez",Yaw Berko na Said Mohamed ambao mara kwa mara walikuwa wakichupia na kuokoa mikwaju hiyo.

Mchezaji Kevin Yondan "Vidic" siku ya leo hakuweza kushiriki katika mazoezi hayo kutokana na kuwa na udhuru ambapo beki huyo aliufahamisha uongozi kwa kushindwa kushiriki katika mazoezi kwa muda ambao ameomba.
Wachezaji wengine ambao hawakufanya mazoezi ni pamoja na kapteni  Shadrack Nsajigwa ambaye pia alikuwa na matatizo,Nizar Khalfan na Nurdin Bakari ambao wameripotiwa kuwa wanaumwa.

Wakati huo huo kiungo wa kimataifa Haruna Niyonzima "Fabregas" anatarajiwa kuwasili nchini na kujiunga na kikosi hicho cha mabingwa wa soka kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati Yanga majira ya mchana.

Akizungumza na website ya Klabu ya Yanga,Kocha msaidizi wa timu hiyo Fred Felix Minziro amesema Niyonzima ndiye mchezaji pekee ambaye alikuwa  hajaripoti katika mazoezi hayo.

Huku straika Mnyarwanda Meddy Kagere akidhibitishwa kuvaa uzi wa kijani na njano msimu ujao. 

No comments:

Post a Comment