Facebook LIKE

Wednesday, June 20, 2012

Bahanuzi,Barthez,Abdul na Nizar kivutio kwa mashabiki wa Yanga leo Kaunda......!

Kikosi cha Mabingwa wa soka wa Afrika Mashariki na Kati, kimeendelea na mazoezi leo katika Uwanja wa Kaunda jijini Dar es Salaam,huku miongoni mwa wachezaji waliosajiliwa msimu huu tayari wakiwa wamejiunga katika mazoezi hayo.
Katika mazoezi hayo aliyekuwa golikipa wa timu ya Simba Mustapha Ally Barthez, mshambuliaji wa timu ya Mtibwa Sugar ya Morogoro Said Bahanuzi na beki wa kulia wa timu hiyo ya Mtibwa Juma Abdul walichangamsha mazoezi hayo yaliyokuwa yakisimamiwa na Fred Felix pamoja na kocha wa magolikipa Mfaume Athuman.
 Wachezaji wengine walioshiriki katika mazoezi hayo ni Oscar Joshua,Stephano Mwasika,Nadir Haroub,Ibrahim Job,Juma Seif,Shamte Ally na Athumani Idd Chuji, wachezaji wengine ni Omega Seme,Jerryson Tegete,Idrisa Rashid,Godfrey Taita,Nizar Khalifan,Hamis Kiiza na Kenneth Asamoah.
Wakati huo huo Kocha Fred Minziro amesema amefurahi kuona kikosi chake kikizidi kuimarika baada ya wachezaji wengi kujiunga katika mazoezi hayo.



No comments:

Post a Comment