Facebook LIKE

Saturday, June 23, 2012

Beki aliyesajiliwa kuziba pengo la Yondan,Simba huyu hapa ni Mkongomani.Huku wakiichapa Toto katika mechi ya kirafiki

BEKI MPYA WA SIMBA,MASOMBO LINO
KLABU ya Simba SC, imefanikiwa kumsajili beki wa kati wa kimataifa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Masombo Lino kutoka Daring Club Motema Pembe.Akizungumzia suala hilo msemaji wa Simba Ezekiel Kamwaga amesema
Beki huyo wa kati ambaye alipiga soka ya uhakika mwaka jana wakati Simba ilipokutana na DC Motema Pembe katika mechi ya mchujo kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika alituatua jana Dar es Salaam na leo imeelezwa limesaini mkataba.  
Ofisa Habari wa Simba SC, Ezekiel Kamwaga ameiambia tovuti ya BIN ZUBEIRY kwamba beki huyo alikuwa ana mazungumzo na Makamu Mwenyekiti wa klabu yao, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ leo baada ya kutua jana na inawezekana leo amesaini mkataba wa miaka miwili.
“Masombo amekuja jana saa mbili usiku, alikuwa ana mzungumzo na Makamu Mwenyekiti, inawezekana leo akawa amesaini mkataba wa miaka miwili kama wameafikiana,”alisema Kamwaga usiku huu.  
Simba, mabingwa wa Ligi Kuu ya Bara, wanamsajili beki huyo kuziba pengo la beki wao hodari, Kelvin Patrick Yondan ambaye amehamia kwa wapinzani, Yanga.

Katika hatua nyingine timu ya Simba imeichapa Toto Africans ya Mwanza katika mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye uwanja wa CCM-Kirumba kwa mabao 2-0.Simba ambayo ipo kwenye ziara kwenye mikoa ya kanda ya ziwa mabao yake yaliwekwa kimiani na winga,Uhuru Suleiman pamoja na kiungo mpya Salim Kinje


Kikosi cha Simba kilikuwa hivi; Waziri, Hassan (Gallas), Ngalema (Omar Waziri), Obadia Mungusa, Haruna Shamte, Amri Kiemba (Edward Christopher), Chanonga, Seseme (Kiggi), Abdallah (Ramadhani Salum), Kinje na Uhuru.

No comments:

Post a Comment