KOCHA wa Yanga, Mbelgiji Tom Saintfiet amewaacha kwenye kikosi
kitakachoshiriki michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati,
Kombe la Kagame kuanzia Jumamosi wachezaji watatu nyota na chipukizi,
Omega Seme, Simon Msuva na Frank Damayo kwa sababu watakuwa na majukumu
ya kitaifa kwa muda mrefu.
Akizungumza na Waandishi wa Habari mchana huu, makao
makuu ya klabu makutano ya Mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam,
Saintfiet alisema kwamba wachezaji hao watakuwa na timu ya taifa ya
vijana chini ya umri wa miaka 20, inayojiandaa mechi ya kuwania tiketi
ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika Julai 29 dhidi ya Nigeria.
“Kwa
mujibu wa kanuni natakiwa kuwaachia wachezaji siku tano kabla ya
mechi, na Jumamosi wanacheza na Rwanda, Jumatatu wanarudiana na Rwanda,
baada ya hapo watakuwa kwenye maandalizi ya mechi na Nigeria, kwa hivyo
sitakuwa nao hata kwenye Nusu Fainali, kwa sababu hiyo nimeamua
kuwaacha,”alisema.
Saintfiet alisema amemtema pia
Nahodha wa klabu hiyo, Nsajigwa Shadrack katika kikosi cha wachezaji 20,
lakini amesema mchezaji huyo ni muhimu na atakuwa naye kwenye Ligi Kuu.
Amewataja wachezaji aliowateua baada ya kushauriana na wasaidizi wake, Freddy Felix Minziro na Mfaume Athumani kuwa ni;
Makipa; Yaw Berko na Ally Mustafa ‘Barthez’
Mabeki;
Juma Abdul, David Luhende, Kelvin Yondan, Nadir Haroub ‘Cannavaro’,
Godfrey Taita, Ladislaus Mbogo, Oscar Joshua na Stefano Mwasyika
Viungo; Athumani Iddi ‘Chuji’, Rashid Gumbo, Juma Seif ‘Kijiko’, Haruna Niyonzima, Shamte Ally, Nizar Khalfan na Idrisa Assenga.
Washambuliaji; Said Bahanuzi, Hamisi Kiiza na Jerry Tegete.
Yanga
ndio mabingwa watetezi wa Kagame, watafungua dimba na mabingwa wa
Burundi, Atletico FC Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kutoka: bongostaz.blogspot.com
No comments:
Post a Comment