Facebook LIKE

Sunday, July 29, 2012

Mshindi wa shindano la Tusker Project Fame 5 huyu hapa..!

MKENYA,RUTH MATETE
Anaitwa Ruth Matete kutoka Kenya na ndio ameondoka na kitika cha million 5 za kenya na mkataba wa kurecord album wenye thamani ya million 10.Ruth ana miaka 26 na amewashinda vijana wa nne wenye uwezo mkali sana ambao ni Joe kutoka burundi ndio namba nne ,akifatiwa na Jackson kutoka Rwanda , Doreen kutoka Kenya akiwa namba mbili . Wakati wanataja washindi mtangazaji wa tusker project fame aliwabakiza wawill Ruth na Doreen aka Miss Probation na kuacha watu wakitabiri yupi atakuwa mshindi . Shindano hili huwa linaanza na washindani 15 na 11 hutolewa mapema kabla ya week ya fainali
Usiku wa fainali, Kundi la vijana wakali kupitia ngoma zao kama party don't stop na Hold it down Camp Mulla walifanya show na Sarakasi dancers.Show ya Camp Mulla ilikuwa nzuri ila malalamiko ya watazamaji ni mavazi na muonekano wa Camp Mulla haujaendana na show hio.

1 comment:

  1. Ruth Really Deserve It, And Besides I saw It Earlier, During Probation and competitions....Other Artist should GET an Example from Her...

    ReplyDelete