Facebook LIKE

Thursday, July 5, 2012

Kuelekea pambano la Wema Sepetu na Jack Wolper,Wema apigwa knockout kabla ya pambano,sababu hizi hapa.....!

WOLPER KUSHOTO NA WEMA KULIA
Kuelekea pambano la masumbwi baina ya wasanii wawili maarufu Bongo katika tasnia ya Movie,Wema Sepetu na Jack Wolper ambalo litafanyika siku ya Sabasaba (Julai 7,2012) hii ni tasmini fupi ya pambano hilo.

Wasanii hao ambao mara kwa mara wamekuwa wakitambiana kwenye sekta tofauti kama kumiliki mali za bei mbaya wanatoka katika kashfa ya kumiliki mali ambazo sio zao,Wema anakashfa ya kutangaza kuwa anamiliki nyumba yenye thamani ya zaidi ya millioni400 za kibongo wakati inasemekana sio nyumba yake.Kwa upande mwengine Jack Wolper yeye anakashfa ya kutangaza kumiliki gari aina ya BMW X6 ya zaidi ya millioni170 za kibongo.

Sasa kwa mtazamo tuliofanya kupitia maoni ya watu mbalimbali inaonyesha kuwa Wolper anapewa nafasi kubwa ya kumchapa mpinzani wake huyo.Baadhi ya sababu ambazo watu wengi wamekuwa wakizitoa ni kama ifuatavyo;

  • Kutokuwa na nywele ndefu kwa Wolper huku Wema akiwa na nywele ndefu,imezoeleka katika ngumi za wanawake kuvutana nywele ni jambo la kawaida kwahiyo watu wengine wamempa nafasi Wolper kutumia mwanya huo kuvuta nywele za Wema pindi refa atakapokuwa anazubaa ulingoni.Huku wengine wakisema Wolper hatoweza kushika nywele za Wema kwasababu ya Grooves ambazo wasanii hao watazivaa kwenye pambano hilo.
  • Sababu nyingine watu wengi walikuwa wanasema ni kuchanika kirahisi kwa Wema ambaye hivi karibuni inaonekana amekuwa akitumia madawa mengi ya mwilini kiasi cha kufanya ngozi yake kuweza kuchanika kirahisi akiwa ulingoni.Mwonekano wa Wema umekuwa tofauti na zamani kutoka na madawa anayotumia huku wengi wakisema hayamfai na anachukiza tofauti na alivyokuwa zamani."Jamani Wema si atachanika kirahisi wakati anapigana na Wolper",mmoja ya watu aliandika kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook huku wengine wakiunga mkono kauli hiyo ya mdada huyo aliyeiandika kwenye facebook huku akiambatanisha na picha ya Wema alivyokuwa zamani na sasa.
  • Pia wanaume wengi wanadai Wolper ni mrembo ila ni kauzu kulinganisha na Wema ambaye wanadai sio kauzu kama Wolper hivyo Wema atapigwa.
  • Na sababu nyingine ni makocha wao ambapo Jack Wolper yupo chini ya Rashid Matumla "Snakeman" na Wema Sepetu yupo chini ya Maneno Oswald "Mtambo wa Gongo".Rekodi zinaonyesha Maneno ambaye ndiye kocha wa Wema mara nyingi huwa anakosa mbinu pindi anapokutana ulingoni na Matumla ambaye ndo kocha wa Wolper sasa watu wamesema Matumla atataka kuendeleza ubabe kwa Maneno kama alivyofanya mara nyingi wanapokutana ulingoni wenyewe kwa wenyewe na sasa kama makocha watu wanadai Matumla ambae ni kocha wa Jack Wolper ataendeleza ubabe wake kwa Maneno ambaye ni kocha wa Wema Sepetu.
*Hayo ni maoni ya baadhi ya watu kutoka katika mitandao tofauti ya kijamii ambao inaonekana wanalisubiria kwahamu kubwa pambano hilo.

No comments:

Post a Comment