Facebook LIKE

Sunday, July 22, 2012

Hii hapa ndo aina ya ndege ambayo Wakenya wamepewa na Marekani katika kupambana na AL SHABAB

Taarifa kutoka Marekani zinaeleza kuwa Wizara ya Ulinzi ya Marekani itaipatia Kenya ndege nane ndogo zisizohitaji rubani, ikiwa ni sehemu ya msaada wa kijeshi kwa nchi za Afrika Mashariki, ili kuzisaidia kupambana na wapiganaji wa Kiislamu wa Somalia, al-Shabaab.
Ndege isiyobeba rubani, drone
HII NDEGE HAITUMII RUBANI NA NI YA KUPELELEZA ZAIDI
Gazeti la Wall Street Journal la Marekani limearifu kuwa Kenya itapata ndege hizo ambazo hazitakuwa na silaha, lakini zinaweza kugundua maeneo yanayofaa kulengwa na ndege au majeshi ya ardhini.
Gazeti hilo limesema ndege zisizokuwa na rubani ni sehemu ya msaada wa Marekani, pamoja na malori, zana za mawasiliano, na silaha kwa Burundi, Djibouti na Uganda.

No comments:

Post a Comment