Facebook LIKE

Tuesday, July 31, 2012

Video ya KIGOMA ALL STARS-Leka Dutigite.EXCLUSIVE


"NEW VIDEO" Mwasiti ft Ally Nipishe-Mapito.


Monday, July 30, 2012

Sikiliza ngoma mpya kali ya Kelly Rowland ft. Lil Wayne-Ice.Wawili hao wamefanya collabo nyingine baada ya ngoma ya motivation


Video ya Ney wa Mitego-Nasema nao,hii hapa..!!



Azam FC wamweka Mrisho Ngassa sokoni rasmi hii ndio bei na sababu za kumweka winga huyo sokoni



MRISHO NGASSA BAADA YA MECHI YA FAINALI KOMBE LA KAGAME

Klabu ya Azam FC inapenda kutoa taarifa rasmi kuwa milango iko wazi kwa klabu yoyote kumnunu mchezaji Mrisho Ngassa kwa gharama ya $ 50,000.

Azam FC imefikia hatua hiyo baada ya mchezaji huyo kuonyesha kutokuwa na mapenzi na klabu hiyo na badala yake kuipenda klabu aliyotoka ya Yanga.
Hivyo uongozi wa klabu unapokea maombi kwa klabu yoyote inayomuhitaji mchezaji huyo.
Azam FC ilitoa nafasi ya upendeleo kwa klabu ya Yanga lakini hakuna ofa iliyoletwa kuhusu, klabu imepokea ofa kutoka Simba kumuhitaji mchezaji huyo.

Ngassa anauzwa siku chache baada ya kukubali kuvaa jezi ya Yanga na kuibusu logo ya timu hiyo, baada ya kumalizika kwa mchezo wa nusu fainali kati ya Azam FC na AS Vita Club ya Congo DRC katika mashindano ya Kombe la Kagame yaliyomalizika Julai 28 mwaka huu.

Sunday, July 29, 2012

Mshindi wa shindano la Tusker Project Fame 5 huyu hapa..!

MKENYA,RUTH MATETE
Anaitwa Ruth Matete kutoka Kenya na ndio ameondoka na kitika cha million 5 za kenya na mkataba wa kurecord album wenye thamani ya million 10.Ruth ana miaka 26 na amewashinda vijana wa nne wenye uwezo mkali sana ambao ni Joe kutoka burundi ndio namba nne ,akifatiwa na Jackson kutoka Rwanda , Doreen kutoka Kenya akiwa namba mbili . Wakati wanataja washindi mtangazaji wa tusker project fame aliwabakiza wawill Ruth na Doreen aka Miss Probation na kuacha watu wakitabiri yupi atakuwa mshindi . Shindano hili huwa linaanza na washindani 15 na 11 hutolewa mapema kabla ya week ya fainali
Usiku wa fainali, Kundi la vijana wakali kupitia ngoma zao kama party don't stop na Hold it down Camp Mulla walifanya show na Sarakasi dancers.Show ya Camp Mulla ilikuwa nzuri ila malalamiko ya watazamaji ni mavazi na muonekano wa Camp Mulla haujaendana na show hio.

Beats kali kutoka K-Styles entertainment contact us for acquirements/needs

Sunday, July 22, 2012

Hii hapa ndo aina ya ndege ambayo Wakenya wamepewa na Marekani katika kupambana na AL SHABAB

Taarifa kutoka Marekani zinaeleza kuwa Wizara ya Ulinzi ya Marekani itaipatia Kenya ndege nane ndogo zisizohitaji rubani, ikiwa ni sehemu ya msaada wa kijeshi kwa nchi za Afrika Mashariki, ili kuzisaidia kupambana na wapiganaji wa Kiislamu wa Somalia, al-Shabaab.
Ndege isiyobeba rubani, drone
HII NDEGE HAITUMII RUBANI NA NI YA KUPELELEZA ZAIDI
Gazeti la Wall Street Journal la Marekani limearifu kuwa Kenya itapata ndege hizo ambazo hazitakuwa na silaha, lakini zinaweza kugundua maeneo yanayofaa kulengwa na ndege au majeshi ya ardhini.
Gazeti hilo limesema ndege zisizokuwa na rubani ni sehemu ya msaada wa Marekani, pamoja na malori, zana za mawasiliano, na silaha kwa Burundi, Djibouti na Uganda.

Saturday, July 21, 2012

Wale wapenzi wa Movie na ChrisBrown hii hapa Trailer ya Battle of the year(3D)


  • Battle of the Year stars Josh Holloway (Lost), Chris Brown (Takers), Laz Alonso (Jumping the Broom, Avatar) and Josh Peck (The Wackness).

Ngoma mpya ya Barnaba-Sijutii kwa niliempata,download na sikiliza hapa


Wednesday, July 18, 2012

Tuesday, July 17, 2012

Yanga yafanya mauaji Kagame yawapiga Wasudan goli 7


Mabao yaliyotiwa kimiani na washambuliaji Mganda Hamis Kiiza,Said Bahanuzi na kiungo Nizar Khalfan yameiwezesha klabu ya Yanga kuibuka na ushindi wa goli 7-1 dhidi ya timu ya Waw Salaam ya Sudan.

Katika mchezo huo ulitawaliwa zaidi na Yanga mshambuliaji Said Bahanuzi ndiye aliyeipatia Yanga bao la kuongoza katika dakika ya 12.Dakika tano baadae Bahanuzi tena alitumbukiza mpira kimiani na kuipatia Yanga bao la pili katika dakika ya 17.Mshambuliaji Mganda Hamis Kiiza alianza kuhesabu mabao yake manne aliyofunga katika pambano hilo katika dakika ya 18,25,30 na 35.Hadi timu hizo zinaenda mapumziko Yanga walikuwa mbele kwa mabao 6-0.

Katika kipindi cha pili Yanga waliwatoa Kevin Yondan,Haruna Niyonzima na Stephano Mwasika na nafasi zao kuchukuliwa na Juma Seif,Rashid Gumbo na Idrissa Rashid.Katika dakika ya 75 kiungo Nizar Khalfan aliipatia Yanga bao la saba.Waw Salaam walijipatia bao lao katika dakika ya 90 ya mchezo

Katika mchezo huo kikosi cha Yanga kilikuwa hivi;

Monday, July 16, 2012

Official video ya Lil Wayne ft.Big Sean-My Hommie Still,hii hapa

Hawa ndio wachezaji 32 wanaowania tuzo ya uchezaji bora Ulaya 2012


  • RealMadrid waongoza kwa kutoa wachezaji wengi
  • ManchesterUnited,Arsenal zatoa mchezaji mmoja kila mmoja
  • Casillas anapewa nafasi kubwa kuchukua tuzo hiyo kulingana na mafanikio aliyoyapata golikipa huyo wa RealMadrid na timu ya Taifa ya Hispania.

ORODHA KAMILI YA WACHEZAJI WANAOWANIA TUZO YA MCHEZAJI BORA ULAYA:
 Player (Club); Sergio Aguero (Manchester City), Xabi Alonso (Real Madrid), Mario Balotelli (Manchester City), Jakub Blaszczykowski (Borussia Dortmund), Gianluigi Buffon (Juventus), Iker Casillas (Real Madrid), Petr Cech (Chelsea), Fabio Coentrao (Real Madrid), Leslie Davies (Bangor City), Didier Drogba (Chelsea), Cesc Fabregas (Barcelona), Radamel Falcao (Atletico Madrid), Joe Hart (Manchester City),

Matoleo mapya ya viatu kwa picha,wale waliosema hawatakuja kuvaa SUPRA kazi kwenu wamerudi tena.......!!!

  • Supra Passion ndo toleo jipya la SUPRA watu wengi wanaonekana kuanza kurudi kwenye SUPRA
  • Pia angalia matoleo mengine ya SUPRA
Supra Passion - Black / Tan
NEW SUPRA PASSION
Supra Passion "Grey"
NEW SUPRA PASSION

Supra Skytop III "Caramel"
NEW SUPRA SKYTOP III "CARMEL"

Video ya interview aliyofanya yule mkali aliyeandika mistari ya BongoFleva kwenye mtihani wa Kidato cha Nne mwaka jana hii hapa hebu mcheki hapa

Sunday, July 15, 2012

Manji mwenyekiti mpya wa klabu ya Yanga,matokeo yote ya uchaguzi mdogo Yanga haya hapa

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa Klabu ya Yanga, Jaji John Mkwawa
 kushoto akiwa na Mjumbe wa kamati hiyo Mzee Mzimba



Yusuf Manji amechaguliwa kuwa mwenyekiti mpya wa klabu ya Young Africans Sports Club, uchaguzi ulioitishwa kujaza nafasi zilizoachwa wazi, kufuatia kujiuzuru kwa baadhi ya wajumbe wa kamati ya utendaji, mwenyekiti na makamu wake.
Akitangaza matokeo hayo, majira ya saa 10:30 alfajiri katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wa klabu ya Yanga Jaji John Mkwawa amemtangza Manji kama mishindi wa nafasi ya uenyekiti kufuatia kupata asilimia 97% ya kura zote zilizopigwa katika nafasi hiyo.
Nafasi ya Makamu Mwenyekiti imekwenda kwa Clement Sanga aliyejipatia asilimia 62% ya kura zote zilizopigwa katika nafasi ya u makamu mwenyekiti.
Abdallah Bin Kleb, Moses Katabaro, Aaron Nyanda na George Manyama  wamechaguliwa katika nafasi ya ujumbe wa kamati ya  Utendaji.
Jaji Mkwawa amewashukuru wana Yanga kwa kuwa wastaarabu na watulivu, kitu kilicholekea kufanyika uchaguzi kwa amani na zoezi hilo kumalizika salama pasipo kuwa na rabsha yoyote.
Matokeo kamili ya wagombea ni:

Nafasi ya Mwenyekiti:
Yusuf Manji (kura 1876)  97.0%,  John Jembele (kura 40) 2.6%, Edgar Chibura (kura 4) 0.24%

Nafasi ya Makamu Mwenyekiti:
Clement Sanga (kura 1948) 62.6%, Yono S Kevela (kura 475) 23%, Ayoub Nyenzi (kura 288) 14%

Nafasi ya Ujumbe:
Abdallah Bin Kleb (kura 1942),Moses Katabaro (kura 1068),Aaron Nyanda (kura 922), Geroge Manyama (kura 682), Beda Tindwa (kura 391), Edgar Fongo (kura 295), Graticius Ishengoma  (kura 247), Jumanne Mwamenywa (kura 251), Justine Baruti (610), Lameck Nyambaya (kura 425), Omary Ndula (kura 170), Peter Haule (441), Ramadhan Said (249), Yono Kivela (123)

Kutokana na matokeo yalivyo hapo juu safu ya viongozi waliochaguliwa ni:
Mwenyekiti: Yusuf Manji,
Makamu Mwenyekiti: Clement Sanga
Wajumbe: Abdallah Bin Kleb, Moses Katabaro, Aaaron Nyanda, Geroge Manyama 

Wale wanapenda kuvaa viatu vya VANS mizigo mipya hii hapa inawahus........!!!

  • Vans California 106 Vulc CA ndio VANS mpya kabisa katika soko la viatu vya VANS
  • Angalia pia na VANS zingine zilizo kwenye chati kwasasa
Vans California 106 Vulc CA “Suede”
Vans California 106 Vulc CA(The Latest/New Vans)
Vans California 106 Vulc CA
Vans Authentic Decon CA | July 2012 Releases
Vans Authentic Decon CA
Vans Cab Lite
Vans Cab Lite

Friday, July 13, 2012

Baada ya wezi kumvamia Wema Sepetu sasa aamua kumuiga mpenzi wake wa zamani Diamond kwa hili

WEMA SEPETU
Pamoja na wajanja kuvamia nyumbani kwake kwa nia ya kumwibia vitu vyake vya thamani  juzi kati na baadaye kushindwa kutimiza adhma yao, Wema Sepetu is here once again kuwa-prove wrong.
Kwa taarifa yako  Diva huyu toka Bongo movies aitwaye  Wema Abraham Sepetu baada ya ku-launch movie yake ya superstar kwa kumdondosha Omotola toka Nollywood industry ya Nigeria at Kempinski na baadaye kufanya family party pale Girafe Hotel,  yuko  tayari kuvunja bank kwa ajili ya kuagiza mkoko mpya aina ya Toyota Prado.
Gari hiyo aina ya Prado itakayo gharimu kiasi cha hela ya Tanzania million sitini mpaka kufika hapa na mambo mengine yote kama usafirishaji na gharama za ushuru wote husika, hiyo itakuwa inakamilisha gari yake ya tatu baada ya ile Mark X na Harrier.Ndiga hii anayotaka kununua Wema Sepetu ni kama ile ambayo mpenzi wake wa zamani,Diamond amenunua hivi karibuni.
HII NDO PRADO YA DIAMOND AMBAYO WEMA ANATAKA KUNUNUA KAMA HIYO

Cheki ndinga mpya aliyonunua rapper The Game.

FERRARI LEATHER>>>DOLA 200,000 MPYA YA GAME
FERRARI LEATHER UMEONA KWANINI WAMEIITA FERRARI LEATHER 
HII NDO FERRARI LEATHER AMBAYO IMEMGHARIMU DOLA 200,000 RAPPER HUYO
THE GAME

Sikiliza nyimbo mpya ya Wiz Khalifa Feat Busta Rhymes - Different Cloth


Wanawake wanaopenda kupendeza na kwenda na wakati hizi zinawahusu....!

  • Wanawake nao kwenda na wakati wanaojipenda hizi picha zinawahusu kina dada.
  • Daily updates za Unique Fashions endelea kutembelea BLOG hii kila siku pamoja na habari zingine za Mjini na Nje ya Bongo.





Thursday, July 12, 2012

Video mpya ya Ben Pol-Maneno maneno,exclusive hii hapa........!!!

Ngoma mpya ya Suma Mnazaleti ft.Ommy Dimpoz-Chukua time,download na sikiliza hapa

Wanyama wa Mjini hizi picha zinawahusu hebu zicheki hapa.........!!!!!SWAG

  • Daily tembelea kwa FASHION>>>>SWAG<<<< za kisasa....!
  • Wale wakina dada Wanyama wa Mjini soon mizigo yenu pia itakuwepo hewani hapa




Kikosi cha Yanga kitakachoshiriki michuano ya Kagame hiki hapa....!

KOCHA wa Yanga, Mbelgiji Tom Saintfiet amewaacha kwenye kikosi kitakachoshiriki michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame kuanzia Jumamosi wachezaji watatu nyota na chipukizi, Omega Seme, Simon Msuva na Frank Damayo kwa sababu watakuwa na majukumu ya kitaifa kwa muda mrefu.
 
Akizungumza na Waandishi wa Habari mchana huu, makao makuu ya klabu makutano ya Mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam, Saintfiet alisema kwamba wachezaji hao watakuwa na timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, inayojiandaa mechi ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika Julai 29 dhidi ya Nigeria.
 
“Kwa  mujibu wa kanuni natakiwa kuwaachia wachezaji siku tano kabla ya mechi, na Jumamosi wanacheza na Rwanda, Jumatatu wanarudiana na Rwanda, baada ya hapo watakuwa kwenye maandalizi ya mechi na Nigeria, kwa hivyo sitakuwa nao hata kwenye Nusu Fainali, kwa sababu hiyo nimeamua kuwaacha,”alisema.
 
Saintfiet alisema amemtema pia Nahodha wa klabu hiyo, Nsajigwa Shadrack katika kikosi cha wachezaji 20, lakini amesema mchezaji huyo ni muhimu na atakuwa naye kwenye Ligi Kuu.
 
Amewataja wachezaji aliowateua baada ya kushauriana na wasaidizi wake, Freddy Felix Minziro na Mfaume Athumani kuwa ni;
 
KIKOSI CHA YANGA KAGAME;

Wednesday, July 11, 2012

Interview aliyofanya mtangazaji wa Clouds FM Diva na BaabKubwa Magazine hii hapa...!!

DIVA LOVENESS LOVE

BK: Ngoma yako “Piga simu” inafanya poa, so when should we expect the video?
DIVA: My video itatoka mwezi wa nane, nishaongea na Adam wa Visual lab na sasa hivi he is kinda of busy na project kadhaa. I will pay myself 1.5 million for this video na tutaisambaza kote nikiwa na my media manager Soudy Brown. So TeamDiva get ready for that.
BK: Who are you dating now?

Huyu hapa mkali DIAMOND akiwa kwenye Tour Zanzibar,pia hiki ndicho alichowauliza mashabiki wake na Watanzania kwa ujumla......!Mnyama unyamani

Angalia hizi picha zaidi ya 25 za msanii Diamond alipokuwa anakwenda Zanzibar kwenye Tamasha za ZIFF kisha mwisho kabisa ya hizi picha kuna swali ambalo Diamond amewauliza nyinyi Watanzania na mashabiki wake kwa ujumla...!Mnyama unyamani "DIAMOND PLATNUMZ"

Kwa vijana wakisasa angalia baadhi ya SWAG materials;clothing,shoes na vingine utapenda hii.Its all about UNIQUE FASHION.

  • Hizi ni kwaajili ya wakaka SWAG ndo habari ya mjini sasa kila siku tutakuwa tunaweka vitu vipya humu kwahiyo jaribu kuwa unatembelea BLOG hii kila siku kupata vitu vipya kila siku vitu vipya.
  • Ni http://www.wenyemji.blogspot.com kwa vitu vya kijanja kila siku vitu vipya.
  • On FASHION AND UNIQUE MATERIALS
  • Tembele DAILY



G-SHOCKS,BEATZ BY DRE,ZINAHUSIKA PIA
YSL KIBONGO BONGO>MSANII JUX VUITTON ANAHUSIKA

Video mpya ya Rich Mavoko-Marry me,hii hapa

Tuesday, July 10, 2012

Ngoma ya Rick Ross-Hold Me Back

Yanga yaichapa JKT Ruvu kuelekea michuano ya Kagame

Mabingwa wazamani wa Tanzania,Dar Young Africans wameichapa timu ya JKT Ruvu 2-0 katika mchezo wa kirafiki uliochezwa leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.Ukiwa na mchezo wa kwanza wa kirafiki kwa kocha mpya wa klabu hiyo Mbeligiji,Tom Saintfiet.

Yanga ambayo inajiandaa na michuano ya Kagame ambayo inaanza wikiendi hii walijipatia mabao yake kupitia beki wake kisiki wa kati,Nadir Haroub"Cannavaro" katika dakika ya 18.Hadi mchezo huo unaenda mapumziko Yanga walikuwa mbele kwa bao hilo moja.Katika kipindi cha pili Yanga walifanya mabadiliko kwa kumtoa kiungo Nizar Khalfan na nafasi yake kuchukuliwa na mshambuliaji mganda Hamis Kiiza,ambaye katika dakika ya 73 ya mchezo huo aliipatia Yanga bao la pili.

Katika pambano hilo Kikosi cha Yanga kilikuwa hivi;

Wale wanyama wa mjini wazee wa mitupio mzigo mpya huu hapa hebu cheki....!


Kuanzia sasa blog hii itakuwa inawaletea updates za FASHION mbalimbali na mizigo mipya ya nguo,viatu na vingine kwaajili ya wale wanyama na wajanja wa mjini wazee wa mitupio kwahiyo usiwe unacheza mbali na blog hii kwa updates za kijanja za mitupio(FASHION) kwa kuanzia leo tunawaletea hii kitu

YSL leopald print sneakers....!