Facebook LIKE

Monday, May 28, 2012

Unaijua gari ya bei nafuu zaidi Duniani,na inayotarajiwa kuwa ya bei nafuu zaidi?Hizi hapa....

 Hii ndo gari ya bei nafuu zaidi Duniani inaitwa TATA NANO zinatengenezwa India na gharama yake kujumuisha na ushuru(TAX) ni kama Dola$2500 za Kimarekani sawa na Shillingi milioni 2.78 ya Kitanzania hapo kujumuisha na kodi zote.
                                                                    TATA NANO(India)
Na hii ndo gari inayotarajiwa kuwa ya bei nafuu zaidi dunia inaitwa Gleagle IG zinatengenezwa China,hawa jamaa wachina wanataka kupiku rekodi inayoshikiliwa na TATA NANO gari za India ambazo ndo za bei nafuu zaidi jamaa wa kichina kweli hawana masihara gari hii itakuwa inagharimu takribani Dola$2220 za Kimarekani sawa na Shillingi milioni 2.35 za Kitanzania pamoja na kodi(TAX) zote.
                                                               GLEAGLE IG(China)

No comments:

Post a Comment