Edit This Menu
Facebook LIKE
Friday, June 22, 2012
Thursday, June 21, 2012
Nurdin Bakary huyoo Azam huku Yanga wakimrejesha kundini winga wao wa zamani......!
Yanga wameendelea kuonyesha mabavu katika usajili baada ya kumsajili Kelvin Yondani, Nizar Khalfan, Barthez, Domayo na wengine wengi, leo taarifa za usajili kutoka klabu hiyo zinasema kwamba klabu hiyo ipo kwenye mazungumzo na klabu ya Azam ili kuweza kumsajili winga wa kimataifa wa Tanzania Mrisho Khalfan Ngassa.

Habari za ndani zinadai kwamba zinadai kwamba Ngassa, Yanga na Azam wapo kwenye mazungumzo ya mwisho na huenda kesho kutakuwa na habari nzuri kwa wapenzi wa Yanga juu ya kurudi kwa kipenzi chao Ngassa mitaa ya Jangwani.
Katika usajili huo Yanga wapo tayari kulipa kiasi kikubwa cha fedha na kumtoa kiungo Nurdin Bakary ili kuweza kumtwaa winga huyo ambaye alishwahi kuichezea Yanga kwa mafanikio kalba ya kuhama kwa uhamisho uliovunja rekodi ya ndani ya usajili baada ya Azam kulipa milioni 60 kwa Yanga na kumtwaa Ngassa

Wednesday, June 20, 2012
Bahanuzi,Barthez,Abdul na Nizar kivutio kwa mashabiki wa Yanga leo Kaunda......!
Kikosi cha Mabingwa wa soka wa Afrika Mashariki na Kati, kimeendelea
na mazoezi leo katika Uwanja wa Kaunda jijini Dar es Salaam,huku
miongoni mwa wachezaji waliosajiliwa msimu huu tayari wakiwa wamejiunga
katika mazoezi hayo.Katika mazoezi hayo aliyekuwa golikipa wa timu ya Simba Mustapha Ally Barthez, mshambuliaji wa timu ya Mtibwa Sugar ya Morogoro Said Bahanuzi na beki wa kulia wa timu hiyo ya Mtibwa Juma Abdul walichangamsha mazoezi hayo yaliyokuwa yakisimamiwa na Fred Felix pamoja na kocha wa magolikipa Mfaume Athuman.
Wachezaji wengine walioshiriki katika mazoezi hayo ni Oscar Joshua,Stephano Mwasika,Nadir Haroub,Ibrahim Job,Juma Seif,Shamte Ally na Athumani Idd Chuji, wachezaji wengine ni Omega Seme,Jerryson Tegete,Idrisa Rashid,Godfrey Taita,Nizar Khalifan,Hamis Kiiza na Kenneth Asamoah.
Wakati huo huo Kocha Fred Minziro amesema amefurahi kuona kikosi chake kikizidi kuimarika baada ya wachezaji wengi kujiunga katika mazoezi hayo.

Tuesday, June 19, 2012
Picha za baadhi ya wachezaji walioanza kuwasili leo YANGA hizi hapa,Mwape nae ndani angalia hapa...!!
![]() |
| Beki Ibrahim Job akiwa na mwanachama wa klabu hiyo |
![]() |
| Kocha wa makipa Mfaume Athumani kulia akiwa Kaimu Kocha Mkuu, Freddy Felix Minziro leo Jangwani. |
![]() |
| NDANI YA GHETTO; Chumbani kutoka kulia ni Godfrey Taita, Julius Mrope, Nadir Haroub 'Cannavaro' na Stefano Mwasyika aliyeipa kisogo kamera. |
![]() | ||
| Pius Kisambale |
Subscribe to:
Posts (Atom)