Facebook LIKE

Sunday, May 27, 2012

Ommy Dimpoz:Sitaki bifu na msanii wowote na sina bifu na Cyrill

Msanii anayetamba na nyimbo zake za nai nai pamoja na baadae OmmyDimpoz amesema kuwa hana bifu na msanii mwenzake kutoka kundi la WAKACHA,Cyrill aka Kamikaze na pia amesisitiza kuwa haitaji na wala hatarajii kuwa na bifu na msanii wowote kwani hiyo itafanya kushusha mziki wake.Hivi karibuni OmmyDimpoz alisikika kwenye baadhi ya vyombo vya habari akimkashifu msanii Cyrill kuwa ni msanii asiyefanya shoo.Lakini siku chache baadae kiongozi huyo wa kundi la WAKACHA nae alijibu mapigo kwa kusema;OmmyDimpoz anabidi ajipange pindi anapofanya interview na sio kukurupuka tuu,pia Cyrill akaendelea kwa kusema kuwa Dimpoz anashepu ya kike.

Hii yote inasemekana ni kutokana na wasnii hao kuwa walikuwa na shoo siku moja kwenye kumbi tofauti so Cyrill alimkashifu OmmyDimpoz kuwa alitaka kumfanyia hujuma BASATA kwa kutangaza kuwa Cyrill sio MTANZANIA na alikuwa hana kibali cha kufanya shoo ili shoo yake(Cyrill) isifanikiwe ila shoo zote mbili zilifanyika.

Ngoma ya MTOTO MLITO sasa kideoni

Baada ya kutamba kwa ngoma yao redioni wasanii Nas3 pamoja na RicciBoi(KingKapita) sasa wapo kwenye hatua za mwisho za kukamilisha video ya track hiyo wasanii hao ambao hapo kabla walitamba na ngoma yao ya Achaaaa ambazo zote kwa pamoja zimerekodiwa na mtayarishaji Mensen Selekta.Location ya ilipofanyikia video hiyo ni katika jengo la BenjaminMkapa Towers jiji Dar es salaam.

Hii ndio gari anayomiliki mchezaji wa klabu ya Yanga,Shaban Kado.

Golikipa ya Yanga Shaban Kado hivi karibuni aliweka kwenye mtandao wa kijamii wa facebook gari yake ambayo anaimiliki.