Edit This Menu
Facebook LIKE
Sunday, September 23, 2012
Sunday, September 2, 2012
Saturday, September 1, 2012
MAKALA:Mbwana Samatta;"Realmadrid walinifuata Kinshasa."(Imeandikwa na Edo Kumwembe)
EDO KUMWEMBE, ALIYEKUWA LUBUMBASHI
NI swali linalowaumiza Watanzania wengi.
Je, Samatta anaweza kuuzwa kwenda kucheza Ulaya?
Watanzania wanatamani kumuona Samatta akiendeleza ndoto zake licha ya sasa kuwa staa wa TP Mazembe.
Wengi wangetamani kumuona akicheza moja kati ya ligi kubwa barani Ulaya, iwe Hispania, England, Ufaransa, Italia au Ujerumani.
Nikiwa na Samatta tukielekea katika sehemu moja ya chakula cha mchana kinachopikwa na Watanzania inayoitwa Parachute, Samatta anaonekana kuwa na hisia zile zile za Watanzania.
"Bado nina kiu ya kucheza Ulaya.
Mimi hapa naona napita kwa sababu natamani sana kukipiga Ulaya.
Najua Watanzania wanachotaka na mimi bado sijabadili msimamo wangu, nikipata nafasi ya kucheza Ulaya tu namlilia Moise Katumbi.
Mtu mwenyewe anaonekana kuwa na huruma kidogo," anasema Samatta huku Thomas Ulimwengu akicheka.
Hili la Katumbi ndilo linaonekana kuwa kikwazo kikubwa katika mazungumzo. Hata Samatta mwenyewe anakiri kwamba Katumbi ni tatizo kubwa kwake kuuzwa Ulaya.
"Nimezungumza na Katumbi kuhusu mimi kucheza Ulaya lakini anaonekana hataki kabisa kusikia habari za mimi kuuzwa.
Kuna wakati aliniambia wazi wazi kwamba timu inayonitaka lazima iilipe Mazembe kiasi cha Euro 10 milioni.
Mimi sina thamani hiyo na wala sidhani kuna mchezaji anayecheza Afrika ana thamani hiyo.
"Nadhani hapo nia yake ni kutoniuza. Eti brother, haiwezekani timu itoe Euro 10 milioni kwa ajili yangu.
Nadhani nikimwambia kuwa nataka kuhama lazima kutakuwa na kasheshe," anasema Samatta huku akicheka.
Hata hivyo, Samatta ananishangaza zaidi anaposema kuwa kuna ofa za kutoka Ulaya zimeshafika mezani kwa Katumbi kwa ajili yake.
Ananishangaza zaidi anaposema kuwa hata wababe wa Hispania, Real Madrid walishatuma maskauti wao wamtazame.
"Katumbi aliwahi kuniambia kuwa maskauti wa Real Madrid walisafiri kuja kunitazama wakati tunacheza na Vita katika Ligi Kuu yetu hapa Congo.
Ilikuwa mechi tuliyocheza Kinshasa, lakini siku ile mimi sikucheza vizuri kwa hiyo sidhani kama walivutiwa au vipi," anasema Samatta.
Pamoja na hali hiyo, Samatta anakiri kwamba ili mchezaji wa Mazembe atimize ndoto zake za kucheza Ulaya ni lazima akubali kuona kipato chake cha pesa kinapungua, labda kama akisajiliwa na timu kubwa barani Ulaya.
"Hata hivyo, braza ukihama Mazembe kwenda Ulaya inabidi uende timu inayoeleweka, kama ukienda timu ya kawaida pato lako litapungua sana kwa sababu Mazembe inalipa posho nzuri kuliko hizo timu za Ulaya.
"Unamuona huyu Kabangu (kiungo wa Mazembe aliyeuzwa kwenda Anderlecht misimu miwili iliyopita) amerudi hapa na ameniambia amerudi kwa sababu hapa wanalipa vizuri kuliko Anderlecht. Yupo hapa nadhani unamuona ameshaongea na Katumbi na ameanza mazoezi.
"Hapa tukishinda mechi kama hizi za kimataifa katika Ligi ya Mabingwa, Katumbi anaweka dola laki tatu mezani (Sh 450 milioni). Tunakuwa watu kama 25 na tunagawana pesa zote hizo.
Sasa kwanini tusiendeshe magari haya? Nadhani kuna klabu za Ulaya hazijafikia posho hizi.
"Hata Katumbi mwenyewe amewahi kuniambia kuwa nikitoka hapa kama naenda Ulaya inabidi niende kucheza timu kubwa iliyo juu ya Mazembe hata kwa mapato."
Kwa fedha alizonazo Katumbi, ambaye pia ni Gavana wa Jimbo la Katanga, huku mara zote akiwa anaonekana katika televisheni akifanya shughuli mbalimbali za Serikali, namuuliza Samatta kama huwa anapata muda wa kuzungumza na Katumbi.
"Huwa ananipigia simu mara nyingi. Lakini mpaka yeye awe na jambo lake au ajisikie. Katumbi ana mambo mengi, mara utasikia yuko Ubelgiji mara kesho asubuhi unamuona Lubumbashi.
Mimi nikimpigia simu haipokelewi, inaita tu. Halafu anaweza kunipigia hata saa nane usiku. Ni mtu mkubwa sana hapa."
Baada ya muda tunaenda Western Union ambapo Samatta anatuma pesa kwa baba yake nyumbani Tanzania.
Ni kiasi kikubwa cha fedha, lakini huo unabakia kuwa utaratibu wake wa kila mwezi.
"Huwa natuma fedha nyumbani kila mwisho wa mwezi.
Ni kitu cha kawaida, Mzee Samatta lazima ajivunie kuwa na mwanaye au vipi braza? Ndiyo maisha yalivyo, tunapata baraka za wazee."
"Hawa wachezaji wa Zambia kina Kalaba, Sunguluma, Sinkala ikifika mwisho wa wiki wanaendesha magari yao kwenda hapo Ndola, si mbali ni mwendo wa saa moja tu, mimi na Thomas (Ulimwengu) inabidi tutume fedha tu nyumbani kwa sababu hatuna uwezo wa kurudi Tanzania mara kwa mara."
Asubuhi ya siku ambayo natakiwa kuondoka inafika. Lakini wote watatu, mimi, Samatta na Ulimwengu tunafunga mabegi.
Wao mabegi yao yanalazimika kusafiri kwa basi kwenda Ndola ambako timu itaweka kambi, lakini wachezaji watasafiri jioni kwenda huko na ndege yao binafsi.
Tunafika mpaka mazoezini kwa ajili ya kuwaacha na kisha nichukue gari la Samatta kupelekwa uwanja wa ndege kuwahi ndege ya saa nne asubuhi.
Tofauti na siku nyingine, safari hii hatupaki ile sehemu ambayo Samatta huwa anapaki gari mazoezini. Hii ni kwa sababu Mfalme Mputu anaweza kutuzuia na nikachelewa kwenda uwanja wa ndege.
NI swali linalowaumiza Watanzania wengi.
Je, Samatta anaweza kuuzwa kwenda kucheza Ulaya?
MBWANA SAMATTA |

Subscribe to:
Posts (Atom)